The House of Favourite Newspapers

Za Chembe Lazima Ukae…Ni Aibu Uwoya Kuishi Kwa Kiki

0
Staa wa Bongo, Irene Uwoya.

KITU kimoja ambacho waigizaji wa filamu Bongo wanakitambua ni kuwa kazi hiyo hailipi kwa sasa. Labda kwa waigizaji wakubwa wenye majina yao kidogo afadhali, lakini waliobaki, ni kuuza sura ili kutengeneza fursa. Na hii unaweza kuithibitisha kama utamzungumzia mtu kama Irene Pancras Uwoya kwa mfano.

 

Ni mmoja kati ya wacheza filamu wenye kufahamika sana nchini, lakini ukiangalia filamu alizoshiriki na aina ya maisha anayoishi, hazifanani hata kidogo. Simaanishi anaishi maisha mabaya, hapana. Ni kuwa hayafanani na wingi wa filamu alizocheza. Katika umri wake wa miaka 29 (amezaliwa Desemba 18, 1988), Irene ameshacheza zaidi ya filamu 36, ambazo kama angekuwa staa kule Nollywood, angekuwa mtu tofauti kabisa.

Irene Uwoya na Dogo Janja wakifanya yao.

Na unapomzungumzia huyu, unasema juu ya mmoja kati ya waigizaji wakali wa kike katika daraja la kwanza Bongo. Ndio, Uwoya yupo levo hiyo, akiwa na wenzake akina Wolper, Wema, Aunt Ezekiel, Kajala, Shamsa, Johari, Monalisa, Chuchu, Riyama na wengine wa aina hiyo.

 

Majina makubwa ya waigizaji wa kike Bongo hayamaanishi hela tofauti na wale wa Nigeria, ambao ni wazuri katika kamera na kwenye akaunti zao.

 

Mastaa kama Gennevieve, Omotola Jalade, Mercy Johnson, Rita Dominic kwa kutaja wachache, wana mkwanja mrefu balaa, unatokana na kazi zao na mikataba mbalimbali ya matangazo. Uwoya, ambaye alipata jina kubwa katika filamu aliyocheza na wababe wa filamu za Bongo, marehemu Steven Kanumba na Vincent Kigosi ‘Ray’ iitwayo Oprah mwaka 2008, anaishi kikawaida kama wanavyoishi wasichana wenzake ambao kibongobongo tunawaita mastaa.

Usipitwe na Matukio, Install App Yako ya Kijanja na Namba Moja Tanzania ya Global Publishers

Android ===>Google Play

iOS ===>Apple Store

Kilichonivutia kumzungumzia, ni baada ya drama kali ya mwishoni mwa wiki iliyopita, ile ambayo watu wa mjini wanaita kiki, alipopata ‘coverage’ kubwa yeye na Dogo Janja, wakisema wameoana. Kuna mengi yanasemwa, wengine wakisema ni kweli, wengine filamu na baadhi wakidai ni video ya mwimbaji ‘aliyepotea’ Keisha.

 

Kama nilivyosema pale mwanzo, maisha ya mastaa wetu wengi hayafanani na vile tunavyowaona. Vyovyote itakavyokuwa, iwe ni kweli ameoana na Janjaro, filamu au video, kitu cha msingi hapa ni kwamba staili yake hii, haifanani naye hata kidogo.

 

Kwa mfano tuseme ni filamu, hivi kazi yote hiyo inahusu harusi tu? Unaitangaza filamu kwa picha moja, tena inayozua mshangao badala ya kuhamasisha? Msingi mzima wa wao kuachia picha na uzushi huo ni ule ukweli kuwa wengi wangepatwa na mshangao wa ndoa hiyo, hasa kwa sababu ya umri wa Janjaro. Kama filamu unataka ivutie kwa sababu ya mtu mmoja, basi bila shaka haina ubora wa kiwango tunachokitegemea. Amekosa ubunifu wa kutengeneza kazi bora, amebaki kuamini katika majina.

 

Kwa mawazo yake, watu watamiminika kuitafuta filamu hiyo kwa sababu waone harusi ya mastaa hao ilivyokuwa, halafu? Kama ni video ya wimbo wa Keisha, ni vizuri, lakini kwa nini kuitoa picha hiyo kwanza?

 

Wasimamizi wa msanii huyo wanajua mtu wao kapotea, wanataka kumrejesha, sasa anawezaje kure
jea kwa kishindo kwa ndoa ya hawa wawili kama kazi yake (wimbo) ni bomu? Watu wake wa masoko wanatembea kwenda mbele, lakini wakiwa wamegeuza vichwa nyuma, hawaoni. Video haiwezi kubebwa na ndoa ya watu wasiohusika na wimbo na ukategemea ‘ita-hit’. Lakini pia kuna wengine wanasema ni kweli Uwoya ameolewa na Dogo Janja, maana wanajua kuwa Janjaro amekuwa ‘akimega’ kisela kwa muda mrefu.

 

Kama ni kweli, siyo mbaya, lakini haimkai vizuri mtu kama Uwoya. Wanasema mapenzi hayana umri, lakini hayohayo mapenzi yana soni, ndiyo maana yanafanyika sirini. Kwa hadhi ya msanii kama Uwoya, ni aibu kuishi maisha ya kutegemea kiki, kwa sababu hayana maana. Huu ni mtindo wa kivivu uliobuniwa na watu wanaoshindwa kufikiri, ndiyo maana utakuta wakati mwingine kiki zao zinakuwa za kijinga hadi zinaboa.

NA OJUKU ABRAHAM, +255 719 786 355

Usipitwe na Matukio, Install App Yako ya Kijanja na Namba Moja Tanzania ya Global Publishers

Android ===>Google Play

iOS ===>Apple Store

Leave A Reply