The House of Favourite Newspapers

Wema Aliamsha Dude Kwa Marafiki wa Bwana’ke

0
Muigizaji Wema Sepetu.

 

Siku chache baada ya picha za muigizaji Wema Sepetu na bwana’ke mpya aitwaye Bakari Kila akiwa bafuni kuvuja, mrembo huyo amedaiwa kulianzisha kum­saka ‘snichi’ aliyezivujisha.

Wema Sepetu na bwana’ke mpya aitwaye Bakari Kila wakiwa bafuni.

 

Picha za Wema na Kila wakiwa bafuni zilivuja wiki kadhaa zilizo­pita katika gazeti ndugu na hili la Ijumaa Wikienda ambapo kwenye picha hizo, Wema alionekana akiwa amevalia kanga moja huku akimpiga busu motomoto Kila.

Mara baada ya ubuyu huo kuanikwa gazetini, chanzo makini kimeeleza kuwa, kuliibuka tafrani la aina yake wakati Wema alipokuwa akihaha kumtafuta mchawi.

 

“Unajua Madam (Wema) ni kama alichanganyikiwa. Alishindwa kung’amua hasa nani ni mdudu mtu ambaye alivujisha picha hizo. Maz­ingira ya picha hizo walipiga wakiwa wawili, yeye na mpenzi wake tena kimahaba zaidi.

Wema Sepetu akiwa katika pozi.

“Anajiuliza sasa kama aliyepiga ni yeye na picha hizo alikuwa nazo yeye na mpenzi wake, ni nani kazivujisha? Sasa kwa sababu hana uhakika, an­ampigia tu kila mtu ili kumpa msala. Yani marafiki wa jamaa yake wana­koma sasa hivi,” kilisema chanzo hicho cha uhakika.

Wakifanya yao.

Kikizidi kumwaga ubuyu, chanzo hicho kiliweka bayana kuwa, mrem­bo huyo hakumaindi sana zilipovuja zile picha za awali akiwa amekaa kwenye kochi lakini zilipovuja hizo mpya za chumbani, alichanganyiki­wa sana kumsaka mchawi.

 

“Unajua hizi mpya ziko romantic sana. Walikuwa nazo wao wawili tu, yeye na bwana wake sasa anajiuliza ni nani amezitoa hadi zikawafikia Global?,” kilisema chanzo hicho.

Kuonesha kwamba amekerwa na kuvuja kwa picha hizo, Wema alione­sha masikitiko yake kupitia kwenye mtandao wa Instagram ambapo alilalamika kuwa mtu aliyemuamini ndiye aliyevujisha hizo picha.

 

Licha ya Amani kuona povu la Wema mitandaoni akimlaumu aliye­vujisha picha hizo (si ambaye amezi­vujisha Global), lilijaribu kumvutia waya Wema ili kumsikia kama ana lolote kuhusiana na picha hizo, simu yake iliita bila kupokelewa.

Leave A Reply