The House of Favourite Newspapers

Ronaldo Awatuliza Mashabiki

0
Mchezaji wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo.

CRISTIANO Ronaldo

 

Ronaldo anayechezea Real Madrid, Jumatano wiki hii alipiga mashuti matano langoni kwa Tottenham Hotspur katika mechi ya Ligi ya Mabingwa ambayo Madrid ilifungwa mabao 3-1.

 

Straika huyo mshindi wa Tuzo ya Mwanasoka Bora wa Fifa, amefunga bao moja tu katika mechi tatu zilizopita na tangu Septemba 26, mwaka huu hajaweza kufunga zaidi ya bao moja.

 

“Takwimu zangu hazijalishi. Mimi ni mtulivu,” alisema Ronaldo na kuongeza; “Siku hizi watu hawaangalii unatoa mchango gani katika timu, wanataka mabao tu, hapo ndipo zilipo takwimu.

 

“Najua nitafunga na ukitaka kuona mabao yangu zaidi nenda Google kaandike ‘Mabao ya Cristiano’, utayaona mengi tu.”

Katika La Liga msimu huu, Ronaldo ana bao moja, lakini kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya anaongoza akiwa na mabao sita.

Leave A Reply