The House of Favourite Newspapers

Madee Kiki Waachie Wasanii Wachanga!

0
Staa wa Bongo Fleva, Hamad Ally ‘Madee’.

HAMAD Ally ndilo jina lake, msela mmoja wa Manzese jijini Dar, ambaye kabla hajajiingiza katika muziki, hakukuwa na mtu anayemfahamu. Lakini alipoanza kujihusisha na muziki huo mwanzoni mwa miaka ile ya 2000, akiwa miongoni mwa wasanii waanzilishi wa kundi la Tip Top Connection, ndipo alipoanza kufahamika kwa mashabiki.

 

Madee ndilo jina lake la kisanii na ni mmoja wa mastaa wakubwa wa Bongo Fleva katika kizazi cha sasa. Anajiita rais wa Manzese katika sanaa, akigombania na rapa mwenzake, Nay wa Mitego.

 

Unapowazungumzia vijana ambao wametumia vizuri vipaji vyao kujiweka sawa kimuziki na kimaisha, huyu hawezi kukosa katika orodha yako. Kwanza kile kitendo cha kudumu katika top ten kwa muda aliokaa, ni jambo la kujivunia kabisa, kwa sababu wanamuziki wengi walioibuka pamoja naye, wamekwama.

 

Ameshafanya nyimbo nyingi zilizofanya vizuri ndani na nje. Lakini hata hivyo, baadhi ya vibao vilivyovuma sana ni pamoja na kile cha Nani Kamwaga Pombe Yangu, ambacho licha ya kuwa ni kimekaa kikatuni, lakini kinatoa ujumbe na kuchezeka.

 

Kazi zake zingine kutaja kwa ufupi ni pamoja na Sheedah, Vuvula, Tema Mate Tuwachape na Hela ambao bado unasumbua katika anga la muziki huo wa kizazi kipya.

 

Moja kati ya vitu vikubwa am­bavyo aliwahi kuvifanya Madee, ni kumleta Dogo Janja ‘Janjaro’ jukwaani akiwa bado mdogo kabisa. Ni wasanii wachache wenye vipaji pia vya kugundua uwezo wa wengine katika kufanya kazi hiyo, kwani licha ya kuwa yeye ni mkazi wa Dar es Salaam, aliweza kuuona uwezo wa Janjaro alipokwenda Arusha, licha ya jiji hilo kuwa na wasanii wengi katika historia ya Bongo Fleva.

 

Hata hivyo, kuna jambo moja amenisikitisha sana Madee am­baye pia amesababisha nikum­buke ishu nyingine kama hiyo, wakati ule akitoa kibao chake cha Hela, ilipoonekana sintofa­hamu kubwa kuelekea kutoka kwa wimbo huo, lakini baadaye ikabainika kuwa lilikuwa ni bifu lililotengenezwa mahususi ili kuu-push wimbo huo.

 

Hivi sasa Madee amesimama na kusisitiza ukweli wa ndoa ya filamu kati ya kijana wake, Dogo Janja na Irene Uwoya. Mara kadhaa, kwa kuamini kuwa yeye ndiye ‘kaka’ wa dogo huyo wa Arusha, ame­pigiwa simu na waandishi na kusisitiza kuwa ni kweli wawili hao wameoana.

 

Ambacho hakina shaka ni kuwa Madee ametengeneza kiki hii ili kuipa uhai filamu inayotayarishwa, bila kujali kama ina ubora wa viwango au la.

 

Ninafa­hamu kuwa kila mch­ezo una kanuni zake, kama am­bavyo sasa im­ekuwa kwa baadhi ya wasanii wa nyumbani kuwa bila hizi kiki zao, kazi haitoki.

 

Lakini ninaamini pia kiki hizo zinafanywa na wasanii wachanga, wasio na ‘fanbase’ kubwa kwa vile ha­waamini namna gani itakuwa sokoni.

Najua filamu inayotengenezwa Madee anaifahamu na bila shaka, alikuwa mmoja wa watu wali­opendekeza waigizaji wa kuifanya. Akamchagua Irine Uwoya na kijana wake, je, hakuamini katika ubora wa uigizaji wao?

Msanii mkubwa kama Madee unaposimama mbele ya ‘mic’ na kudanganya umma, ni jambo la aibu. Sanaa ya filamu inakufa kwa sababu waigizaji wake wanaleta sanaa hata katika maisha yao binafsi, kitu ambacho huyu rais wa Manzese naye anakileta.

Pengine ilikuwa ni dili ndani ya dili ili mwenye filamu aongeze fedha ya promo, lakini mbona kuna aina nyingi tu ya matangazo ambayo yangeweza kumuachia heshima yake bila kuleta huu utoto na kuleta tija?

Huu utoto ungemuacha nao mtoto mwenyewe Janjaro ahangaike nao, wewe kama mtu mzima, ungesema tu kuwa ni filamu, mbona Uwoya mwenyewe kwa kuwa anajitambua ameweka wazi kuwa ni igizo na amelipwa fedha nyingi?

Madee, hebu achana na hiyo tabia inayotaka kukukolea, tengeneza kazi nzuri kisha waachie mashabiki waamue. Umewahi kumuona Jay am­etengeneza kiki kwa kazi yake mpya? Lady Jaydee je? Kina AY na Mwana- Fa wanatangulizaga vituko kama hivi ili kazi zao zi-shine?

Za chembe Lazima Ukae OJUKU ABRAHAM, +255 719 786 355

Live: Kipindi cha Maswali na Majibu leo Nov 10, 2017 Mkutano wa Tisa

Leave A Reply