The House of Favourite Newspapers

JPM Atoa Onyo Uchaguzi Mkuu wa UWT – CCM (Video)

Rais Magufuli akihutubia.

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. John Pombe Magufuli ametoa onyo kali kwa watakaojihusisha na rushwa wakati wa mchakato wa uchaguzi mkuu wa Viongozi wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) ndani ya CCM.

 

Hayo ameyasema leo Desemba 8, mjini Dodoma wakati akizindua mkutano wa tisa wa wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), CCM kueleza kuwa hatosita kumchukulia hatua mtu yeyote atakayebainika kutumia mbinu za ujanjaujanja ikiwemo rushwa ili achaguliwe.

 

 

VIDEO: HOTUBA YA RAIS MAGUFULI

 

“Nikigundua kulikuwa na ukiukwaji katika uchaguzi sitasita kuchukua hatua, na hii ni kwa UVCCM, UWT, Wazazi na jumuiya nyingine, kwa sababu mimi sikupita kwa rushwa kama kuna mchezo huo mchafu ulifanyika tutakaa na tutafuta huo uchaguzi. Mchaguze viongozi kwa kumtanguliza Mungu atakayekuwa mtetezi wa kina mama siyo wa tumbo lako, mchague kiongozi anayethamini kanuni na Katiba ya CCM.

 

“Haiwezekani tukawa na viongozi ambao wametekwa na watu wengine kwa maslahi ya mambo fulani, niwaombe Wana-CCM wenzangu tunafahamu UWT iliyokuwa ya kina Sophia Samba siyo UWT tuliyo nayo sasa. Nawapenda kina mama naomba mnisaidie katika hili mtakayemchagua awe anajitambua kwamba kuongoza zi ufalme ni kuwatumikia anaowaongoza.

“Nawapenda kina mama naomba mnisaidie katika hili mtakayemchagua awe anajitambua kwamba kuongoza zi ufalme ni kuwatumikia anaowaongoza. Msichague mtu kwa ukabila, ukanda wala mtoa rushwa mkumbuke ahadi ya CCM kuwa rushwa ni adui wa haki, sitapokea wala kutoa rushwa.

 

“Kinamama wanafanya kazi vizuri sana ndiyo maana nilimteua Mama Samia Suluhu Hassan kuwa mgombea mwenza wangu mwaka 2015, Naibu Spika, Tulia Akson, Mama Salma Kikwete wanafanya vizuri bungeni nitaendelea kuwateua kinamama,” amesema Rais Magufuli.

 

BREAKING NEWS: Anna Mghwira Atangaza Kujiunga CCM

 

Comments are closed.