The House of Favourite Newspapers

Wolper Kuonesha Kufuli Huo Ni Ushamba!

Jacqueline Wolper.

 

JACQUELINE Massawe ndilo jina alilopewa na wazazi wake alipozaliwa kule kwao Moshi mkoani Kilimanjaro, lakini umma wa Watanzania na wadau wa filamu Afrika Mashariki wanamtambua kama Jacqueline Wolper.

 

Ni muigizaji mzuri anayejua nini anafanya akiwa kazini kwake na hiyo ndiyo sababu inayomfanya kuwa mmoja wa waigizaji mahiri katika sanaa hiyo hapa Bongo. Mwenyewe anamshukuru Lucy Komba, muigizaji mwenzake ambaye naye anafanya vyema pia, kumuingiza kwenye ulimwengu wa filamu.

 

Tofauti na waigizaji wenzake wengi wa kike, Wolper anaweza ku-fit katika maeneo mengi, yakiwemo yale yanayowahitaji wanawake ‘waliodata’ au majike dume, ambao wanaweza kufanya vurugu zinazowatisha hata wanaume.

Tazama filamu zake kama Tom Boy au Dereva Taxi ndiyo utajua ninachomaanisha. Akiamua kuwa msichana mrembo katika filamu utapenda swaga zake, lakini pia akisema awe mwanamke nunda, utafurahi na roho yako.

Kifupi, Jacqueline Wolper ambaye pia anajulikana kama Wolper Gambe, ni miongoni mwa waigizaji ambao mchango wao katika tasnia hii hauwezi kubezwa hata mara moja, kwa sababu kama ni wingi wa kazi au umahiri anao wa kutosha.

 

Kama maisha ya waigizaji wa kibongo yangekuwa yanakwenda sambamba na kazi zao kimaslahi, basi kwa filamu zake zaidi ya 40 ambazo ameshacheza hadi sasa, Wolper angekuwa mmoja wa waigizaji wenye mkwanja mrefu hapa nyumbani, kwani mtu kama Gennevive Nnaji wa kule Nigeria, kwenye akaunti yake zinasoma kama bilioni 2 za madafu!

 

Ndiyo maana Wolper amekuwa maarufu sana magazetini kwa vituko na skendo, hasa za kimapenzi kuliko ambavyo mashabiki wake wangetegemea.

Juzikati, binti huyu alikuwa na sherehe ya kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa (ambazo hata hivyo siku hizi zimekuwa adimu kidogo), iliyofanyika katika ukumbi mmoja jijini Dar es Salaam.

 

Kama kawaida, alialika ndugu, jamaa na marafiki na kujumuika nao katika vinywaji, kitu ambacho waalikwa walikifurahia kwelikweli. Hata hivyo, kilichowaacha midomo wazi, ni zile nguo alizovaa.

Gauni moja refu jeusi, ambalo lilikuwa kama nyavunyavu zilizoacha sehemu kubwa ya mwili wake ukionekana. Mtu hakupata taabu kuiona ‘kufuli’ yake, jambo ambalo kwa muda mwingi, lilimfanya aweke mikono yake mbele kujiziba, kana kwamba alivalishwa kinguvu!

 

Sasa hapo ndipo ninapojikuta na maswali mengi yanayokosa majibu. Ni kitu gani kilimfanya avae gauni lile ambalo yeye mwenyewe aliona wazi kabisa linampa shida?

Na bahati mbaya, anavaa gauni la kijinga kama lile, huku akifahamu wazi kuwa kuna watu

 

wanampiga picha ambazo wataziposti katika akaunti zao na hivyo kuonekana kwa watu wengi zaidi jinsi alivyojiachia nusu utupu namna ile!

 

Unaweza kupata picha moja tu kuhusu kioja hiki cha muigizaji huyu, kwamba alifanya hivyo makusudi ili kujitangaza kupitia mitandao. Kujitangaza ili afaidike na nini ni ngumu kujua, lakini kwa kuwa hakushika biashara yoyote mkononi, ni wazi kuwa alikuwa anajitangaza mwenyewe.

 

Pengine alihitaji watu kumuona jinsi mwili wake ulivyo anapokuwa hana nguo, maana wakati mwingine mavazi yanawafanya wawekezaji wasijue kwa uhakika hasa jinsi mtu alivyo. Kama hivi ndivyo, hili siyo jambo la kujivunia hata kidogo, kwa muigizaji kama Wolper ambaye ana mashabiki kila rika!

 

Wakati mwingine Wolper anatakiwa kukua kiakili kwani siyo kila sehemu uwe unatengeneza habari. Umri unakwenda hivyo ni vyema muda mwingine kuuheshimu, kwani kila siku kufanya mambo ya zamani, watu wanaokuheshimu wanashindwa kukuelewa.

 

Na nadhani tamko la hivi karibuni la Rais John Magufuli limekuja kwa wakati muafaka, watu wa aina hii waende huko kwa wazungu wakafanye hayo mambo. Maana kuna wasichana wengi hivi sasa wanaona mitandao kama sehemu ya kutangaza biashara ya miili yao, hii itawahusu sana na wasaidizi wa rais wasirudi nyuma kulitekeleza!

ZA CHEMBE LAZIMA UKAE  NA OJUKU ABRAHAM, +255 719 786 355

Comments are closed.