The House of Favourite Newspapers

Caf Yatangaza Utaratibu Wa Kuchezesha Droo Klabu Bingwa, Shirikisho leo

Shirikisho la Soka la Afrika (CAF) leo litachezesha droo ya makundi ya timu zilizofuzu kucheza Ligi ya Mabingwa makao makuu  leo saa mbili usiku kwenye Hoteli ya Ritz Carlton,  jijini Cairo, Misri.

 

Droo hizo za KlabU Bingwa zitachezeshwa kulingana na matokeo ya timu husika katika miaka mitano  iliyopita kuanzia 2013 hadi 2017.

 

Kwa Ligi ya Mabingwa timu zimepangwa katika makundi manne ambayo ni:

Pot 1: TP Mazembe (DR Congo), Al Ahly (Egypt), Etoile du Sahel (Tunisia), Wydad (Morocco)

Pot 2: Mamelodi Sundowns (South Africa), Zesco (Zambia), Esperance (Tunisia), ES Setif (Algeria

Pot 3: MC Alger (Algeria), KCCA (Uganda), Horoya (Guinea), Mbabane Swallows (Swaziland)

Pot 4: Primero de Agosto (Angola), Township Rollers (Botswana), Difaa El Jadidi (Morocco), AS Port (Togo)

 

Kwa upande wa Kombe la Shirikisho  makundi  yamepangwa kufuatana na matokeo ya timu 32 ambazo timu hizo zimecheza katika miaka mitano iliyopita kama ifuatavyo:

Pot A: El Hilal (Sudan), Saint George (Ethiopia), AS Vita (DR Congo), Zanaco (Zambia)

 

Pot B: USM Alger (Algeria), Supersport (South Africa), Hilal Obied (Sudan), Enyimba (Nigeria)

 

Pot C: ASEC Mimosas (Cote d’Ivoire), Mounana (Gabon), Young Africans (Tanzania), Williamsville (Cote d’Ivoire), Aduana (Ghana), Gor Mahia (Kenya), UD Songo (Mozambique), MFM (Nigeria), Plateau (Nigeria), Rayon Sport (Rwanda), Generation Foot (Senegal), Bidvest (South Africa)

 

Pot D: CR Belouizdad (Algeria), La Mancha (Congo), CARA (Congo), El Masry (Egypt), Niefang (Equatorial Guinea), Wolaitta Dicha (Ethiopia), Fosa Junior (Madagascar), Djoliba (Mali), RS Berkane (Morocco), Raja Club Athletic (Morocco), Costa do Sol (Mozambique), Akwa (Nigeria)

 

Droo ya kwanza itahusisha  mechi kati ya timu za Kundi A na Kundi D. Mchakato huo utarudiwa mara nne.  Baadaye, timu zilizoko Kundi B zitapambanishwa na Kundi C.  Mchakato huo pia utarudiwa mara nne.

 

Baada ya kukamilika, timu nane zilizobaki Kundi C zitapangiwa na timu zilizoko Kundi D. Timu itakayokuwa imebaki katika Kundi C itapambanishwa na timu kutoka Kundi D.  Mchakato huo utarudiwa mara nane kukailisha ratiba

 

Comments are closed.