The House of Favourite Newspapers

Kila La Heri Yanga, Mashabiki Onyesheni Uzalendo

 

KESHO Jumapili saa 1 usiku kwa saa za Tanzania Yanga itaikaribisha Gor Mahia katika mchezo wake wa raundi ya nne ya hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.

 

Mechi hii ni muhimu sana kwa wawakilishi wetu hawa wa Tanzania kwenye michuano ya kimataifa, kwani ukiangalia katika kundi lao ambalo ni D wapo nafasi ya mwisho tena wakiwa na alama moja waliyoipata katika michezo mitatu.

Ni vyema wachezaji wakiingia uwanjani wakiwa wanafahamu kuwa wana deni kubwa ambalo ni lazima walilipe kwa kupata ushindi hapa nyumbani.

 

Ushindi kwenye mchezo huu unamaanisha kuwa sasa Yanga inaweza kuurejesha matumaini ya kuweza kusonga mbele au kumaliza hatua hiyo ikiwa kwenye nafasi nzuri.

Lakini pia Yanga inaweza kufanya vizuri ikiwa itapata sapoti ya kutosha kutoka kwa mashabiki watakaojitokeza kwenye Uwanja wa Taifa kuwashangilia bila kujali matokeo yatakayotokea.

Uzalendo utakaoonyeshwa na mashabiki hao kwa Yanga utawashangaza wageni ambao wanaweza kubabaika na kupoteza mchezo na kama watakuta kuna kundi la Watanzania linawasapoti wao kwanza watatushangaa halafu itakuwa rahisi wao kutushinda.

Ni vyema mashabiki wakafahamu kuwa kuifanyia hujuma Yanga kwenye mchezo wa kesho ni sawa na kujiharibia sisi wenyewe kwani timu hiyo inawakilisha nchi na ndiyo ndugu zetu pekee waliobaki kwenye michuano hiyo ya kimataifa.

Comments are closed.