The House of Favourite Newspapers

DC JERRY MURO AOMBA USHIRIKIANO ARUMERU

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Jerry Muro,  akiongea na wananchi wa Wilaya ya Arumeru.

MKUU wa Wilaya ya Arumeru, Jerry Muro,  jana alifanya ziara ya kikazi na utambulisho kwa watumishi wa Halmashauri  ya Meru  yenye kata 26 na Arusha yenye kata 27 zilizo katika wilaya hiyo.

Muro aliwataka watumishi kufanya kazi kwa kuzingatia mahitaji ya utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambayo anasimamia utekelezaji wake katika halmashauri hizo zenye kata 53.

Katika ziara hiyo aliambatana na Mkuu wa Wilaya ya Monduli, Iddi Kimanta,  aliyekuwa akikaimu Wilaya ya Arumeru, na Katibu Tawala, Timotheo Mzava, na baadhi ya viongozi wa kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya ya Arumeru .

Comments are closed.