The House of Favourite Newspapers

Zahera: Manji Atatupa Ubingwa

Mwinyi Zahera, raia wa DR Congo.

KOCHA Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera, raia wa DR Congo, amewatuliza mashabiki wa timu hiyo kuwa waondoe hofu kabisa kutokana na kurejea kwenye timu mwenyekiti wao, Yusufu Manji kwani malengo yake ni kuipa ubingwa mapema na kuitengeneza Yanga itakayotisha Afrika.

 

Manji inaelezwa amerejea kwenye timu hiyo baada ya kwenda kutoa sapoti katika mchezo wao wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya USM Alger uliopigwa wikiendi iliyopita na Yanga kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1.

 

Akizungumza na Championi Jumatano, Zahera alisema kuwa malengo yake ni kuona anaipa Yanga ubingwa wa msimu huu mapema na kurejea kwa kiongozi huyo kwenye timu kutawaongezea kitu wachezaji wake ambao hata kwenye mechi iliyopita anadai hawakucheza katika ubora aliotarajia wakiwa mbele ya bosi wao huyo.

 

“Unajua malengo yangu kama kocha ni kuona tunakuwa mabingwa, hilo ndilo jambo la kwanza na pili ni kujenga Yanga ambayo itakuwa tishio hapa ndani na Afrika kwa zaidi ya miaka mitatu, jambo ambalo linawezekana kabisa na ukiangalia mwenyekiti amerejea anaweza kutusaidia sana.

 

“Ngoja nikwambie, si umeangalia mechi iliyopita mashabiki wanafurahia timu imecheza vizuri lakini kwangu naona wazi haijafikia katika kiwango ambacho nilitarajia lakini walipapambana na kwa kuwa hakuna mtoto ambaye anafurahia tabu maana kiongozi amerudi kutusapoti, naamini kuja kwake kutanirahisishia kazi ya kusaka ubingwa mapema,” alisema Zahera.

Comments are closed.