The House of Favourite Newspapers

PICHAZ: Mapokezi ya Wasanii wa Wasafi Festival Iringa Usipine

BAADA ya wiki iliyopita Wasafi Festival kuzinduliwa mkoani Mtwara kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Crew ya WCB, leo Ijumaa itakuwa na shughuli moja tu ya kuumiza nyasi za Uwanja wa Samora mjini Iringa.

Nyasi hizo zitaumizwa wakati mashabiki wa muziki watakapokuwa wakipata burudani katika tamasha hilo ambalo sasa limetua mkoani kwao.

Akizungumza na Championi Ijumaa, Mkurugenzi wa Wasafi Classic Baby ‘WCB’, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ alisema kuwa maandalizi ya tamasha lote kwa jumla yamekamilika.

“Nguvu kubwa tuliiweka Mtwara kwa sababu ni mkoa muhimu sana katika historia yetu kama WCB, nasema muhimu kwa kuwa nimekuwa nikiongea mara kadhaa kuwa heshima ya Mtwara kwetu WCB imekuzwa na Harmonize ambaye ndiye msanii pekee tuliyeanza naye kuitambulisha lebo yetu.

 

“Mbali na hilo, pia utaona juhudi za Harmonize ambazo amekuwa akizifanya ili kuhakikisha lebo yetu inaendelea kuonekana siriazi kwa watu wa Mtwara, hivyo hatukuwa na budi kuelekeza nguvu nyingi kule japo simaanishi eti Iringa hatujaweka nguvu kubwa.

 

“Tumejipanga kuhakikisha tunaweka nguvu kwa kila mkoa ambao Wasafi Festival itapita lengo kubwa ni kuwafanya mashabiki zetu tunawaburudisha vya kutosha lakini pia tuhakikishe tunarejesha kidogo tunachokipata kutoka kwao.

“Tukiwa Iringa, tutafanya makamuzi na wasanii wengine waliopo nje ya Lebo ya WCB.

“Tumepanga kwenda mikoa zaidi ya mitano kwa kuwa ni mwanzo tu, ila kama mambo yataenda vyema mwakani tutazunguka nchi nzima.

“Tukishamaliza Ijumaa, tutahamia Morogoro kwenye Uwanja wa Jamhuri ambapo tutakuwa sambamba na wasanii wanaoitambulisha Morogoro kama Afande Sele na Belle 9 ila ukiachilia mbali hao tutatoa nafasi kadhaa kwa wasanii wachanga waliopo mkoani hapo kwani lengo ni kuona vijana wenzetu wanapata nafasi ya kuonyesha vipaji vyao,” alisema Diamond.

Katika shoo ya Iringa, wasanii walio nje ya Lebo ya WCB watakaokuwepo ni, Stereo, Niki Mbishi, Khadija Kopa, Chin Bees, Moko, Young Killer, Dudu Baya na Linah. Kwa Morogoro, wataongezeka Navy Kenzo, Afande Sele na Belle 9.

PICHA/HABARI: MUSA MATEJA – MWARA -GPL

    

Comments are closed.