The House of Favourite Newspapers

Kingwendu Awapa Neno Wanaomzushia Kifo

Rashidi Mwinshehe ‘Kingwendu’

MUIGIZAJI maarufu wa vichekesho Bongo, Rashidi Mwinshehe ‘Kingwendu’ ameyatolea ufafanuzi madai ya kuwa ni mgonjwa wa kufa wakati wowote huku wengine wakizusha kuwa amekufa.

 

Akizungumza na Showbiz, Kingwendu alisema yeye si mgonjwa kama watu wanavyomzushia kwani anaendelea vizuri na sanaa yake hasa ya muziki kwa sababu amekuwa akipiga shoo zake kama kawaida mikoani.

 

“Unajua watu wanaonizushia habari za ugonjwa, mara oo… nimekufa ni wale ambao hawajaniona muda mrefu kwani nafanya kazi zangu binafsi na shoo mbalimbali za muziki huko mikoani, ingawa mimi sishtuki kwani wananitabiria umri mrefu,” alisema Kingwendu.

 

Kingwendu alisema kuwa, ana miaka mingi hajaugua hata malaria na mpaka sasa anapiga shoo mkoani Mwanza katika kuufunga mwaka wa 2018

STORI NA IMELDA MTEMA

 

Comments are closed.