The House of Favourite Newspapers

Mkazi wa Tarime ajishindia Milioni 10 za Tigo Jigiftishe

Mkazi wa Tarime Mkoani Mara Ahia Stephen (kushoto), akipokea mfano wa hundi ya Sh 10m/- kutoka kwa Meneja wa Tigo kanda ya Ziwa Daniel Maino.
Meneja wa Tigo kanda ya Ziwa Daniel Mainoya (kulia) akisisitiza jambo kwa mshindi wa zawadi ya  Sh 10m- katika promosheni ya Tigo Jigiftishe Ahia Stephen (kati kati) muda mfupi kabla ya kumkabidhi zawadi yake.
Mshindi wa zawadi ya wiki ya sh 10m, Ahia Stephen (katikati)akifurahia mfano wa hundi.
…Ahia Stephen (kushoto) akiwapungua wakazi wa mji mdogo wa Tarime waliofika katika viwanja vya stendi ya Tarime kushuhudia akikabidhiwa zawadi yake. Kushoto ni Meneja wa Tigo Mkoa wa MaraAbdillahi Luhorera.

 

 

Mkazi wa Wilaya ya Tarime Mkoani Mara Ahia Stephen, ameibuka mshindi wa wiki katika promosheni ya Tigo Jigiftishe na kujinyakulia kitita cha shilingi milioni 10.

 

Stephen  anakuwa mshindi wa sita wa zawadi ya shilingi milioni kumi baada ya David Mmuni, Iyaka Muinga, Jane Jisandu wote wa Dar es Salaam pamoja na Mbwana Mbela mkazi  wa Mpwapwa mkoani Dodoma na Flora Somba wa Morogoro.

 

Akizungumza muda mfupi baada ya kukabidhiwa zawadi yake wilayani Tarime mwishoni mwa wiki, mshindi huyo aliishukuru kampuni ya Tigo kwa zawadi hiyo na kusena itamsaidia kutimiza baadhi ya malengo yake kwa urahisi.

 

“Naishukuru promosheni hii kwa kunipatia Sh 10m/-. Fedha hii imekuja muda muafaka kwa kuwa itanisaidi kulipa ada za shule kwa watoto wangu na pia itanisaidia kupanua mradi wangu wa ufugaji wa kuku. Natarajia pia kuanza ujenzi na fedha hii itakuwa nia ya msaada mkubwa kufanikisha lengo hili,” alisema.

 

Stephen alisema alifanikiwa kushinda zawadi hiyo kutokana na kutumia huduma za Tigo Pesanikiwa bni pamoja na kutumua pesa, kukunua vifurushi mbali mbali nakuongeza kuwa ilikuwa vigumu kuamini kuwa amejishindia kiasi hicho pesa kwa urahisi alipopigiwa simu kuambiwa kuwa ni mshindi.

 

Kwa upande wake Meneja wa Tigo kanda ya Ziwa Daniel Mainoya, alimpongeza Styephen kwa kuibuka mshindi na kuwataka watu kuendelea kutumia huduma za tigo ili waweze kuingia katika droo ambazo wanayo nafasi ya kujishindia shilingi milioni 50,25 na 15.

 

Kuweza kujishinda mamililioni katika promosheni ya Tigo Jigiftishe ni rahisi sana, haina makato ya pesa wala kujiunga, ukitumia huduma zetu za tigo unaibuka mshindi” alisema Mainoya.

 

Comments are closed.