Yanga, Azam Kucheza Nyumbani FA Cup

Wachezaji wa timu ya Yanga.

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limeiweka hadharani ratiba ya Raundi ya Nne ya Kombe la FA ambapo mechi zake zitachezwa kati ya Januari 25 na 28, mwaka huu.

 

Katika ratiba hiyo inayo­jumuisha timu 32, Yanga na Azam FC zitacheza mechi zao nyumbani sambamba na mabingwa watetezi, Mtibwa Sugar.

Ratiba kamili ya michuano hiyo ipo hivi; Rhino Rangers vs Stand United, KMC vs Pan African, Kagera vs Mbeya Kwanza, Polisi Tanzania vs Lipuli, Yanga vs Biashara, Kitayosce vs Coastal Union, Azam vs Pamba na Singida vs JKT Tanzania.

 

Mtibwa vs Majimaji, Mashujaa vs Mbeya City, Af­rican Lyon vs Friend Rangers, Mighty Elephant vs Namun­go, Alliance vs La Familia, Dodoma vs Transit Camp, Cosmopolitan vs Dar City na Reha vs Boma.

 

Fainali ya mwaka huu imepangwa kuchezwa kwenye Uwanja wa Ilulu ul­iopo Lindi ambapo bingwa ataiwakilisha Tanzania Bara kwenye Kombe la Shirik­isho Afrika msimu ujao.

 

JIUNGE NA FAMILIA YA GLOBAL TV UPANDE MTANDAO WA MAFANIKIO

Bofya hapa kujiunga na familia ya Global TV Club ==> Global TV Family Club

Loading...

Toa comment