The House of Favourite Newspapers

DTB YATWAA UBINGWA WA MASHINDANO YA KIKAPU

Wachezaji wa kikapu kutoka DTB Tanzania wakisherehekea baada ya kuiadhibu NMB kwa pointi 90-73 katika pambano la fainali ya michuano ya Kikapu kwa Taasisi za fedha (Bankers Basketball League) kwa mwaka 2018/2019. Fainali ya pambano hilo ilifanyika Januari 19 kwenye viwanja vya Gymkhana jijini Dar es salaam. DTB-Tanzania walitwaa ubingwa huo bila kupoteza mchezo hata mmoja. Benki zilizoshiriki kwenye michuano hiyo ni pamoja na Azania CRDB, TADB na NMB.
Mlinzi mahiri wa timu ya kikapu ya DTB Tanzania, Frank Mwemezi akipokea kikombe kutoka kwa Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa NMB, Juma Kimori baada ya kuibuka Mlinzi bora wa michuano ya kikapu kwa taasisi za fedha (Bankers Basketball League) kwa mwaka 2018/2019. 
Wachezaji wa timu ya kikapu ya DTB Tanzania wakipiga picha aina ya ‘Selfie’ baada ya kuibuka washindi.
Wachezaji wa timu ya kikapu ya DTB Tanzania wakiwa kwenye picha ya pamoja 

Wachezaji wa kikapu kutoka DTB Tanzania wameifunga NMB kwa pointi 90-73 katika pambano la fainali ya michuano ya Kikapu kwa Taasisi za fedha (Bankers Basketball League) kwa mwaka 2018/2019. Fainali ya pambano hilo ilifanyika Januari 19, 2019 kwenye viwanja vya Gymkhana jijini Dar es salaam. DTB-Tanzania wamechukua ubingwa huo bila kupoteza mchezo hata mmoja. Benki zilizoshiriki kwenye michuano hiyo ni pamoja na Azania CRDB, TADB na NMB.

Comments are closed.