The House of Favourite Newspapers

Namungo waanza kuitisha Yanga

Namungo FC

UONGOZI wa Namungo FC kutoka Ruangwa,Lindi, wanautamani kwa hamu kubwa mchezo wao na Yanga kwenye kombe la FA hatua ya 16 bora.

 

Namungo walitinga hatua hiyo baada ya kuwatwanga Mighty Elephant ya Songea kwa bao 1-0, huku wapinzani wao Yanga wakiwadunda Biashara United ya Mara kwa penati 5-4,baada kuchapana mabao 2-2 ndani ya dakika 90.

 

Akizungumza na Spoti Xtra,mwenyekiti wa Namungo Hassan Zidadu alisema; “Tunawatamani hao
Yanga kwa kiasi kikubwa,hamasa ya wachezaji na mashabiki wa Namungo ipo juu sana tofauti na tulivyofikiria.” “Wana Ruangwa wanausubiri mchezo huo kwa hamu kubwa, ushindi upo kwa Namungo nina uhakika kuwa tutawaondosha Yanga kwenye hatua hiyo,” alisema Zidadu.

Comments are closed.