The House of Favourite Newspapers

Ajibu: Alliance Wagumu Ila Tunawapiga

Ibrahim Ajibu

YANGA tayari ipo Mwanza kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Bara huku nahodha wa timu hiyo, Ibrahim Ajibu akisisitiza ushindi katika mchezo huo mgumu.

 

Timu hiyo, ilitua mkoani hapo saa mbili kamili asubuhi kwa Shirika la Ndege la Air Tanzania wakitokea jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mchezo huo wa ligi dhidi ya Alliance.

 

Yanga inayoongoza ligi ikiwa na pointi 61, kesho Juma­mosi inatarajiwa ku­jitupa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba mkoani humo mchezo unaotarajiwa kujaa upinzani mkubwa.

 

Akizungumza na Championi Ijumaa, Ajibu alisema mchezo huo una umuhimu mkubwa kwao katika kuhakikisha wanaendelea kukaa kileleni ili wawaache wapinzani wao kwa idadi kubwa ya pointi.

Ajibu alisema ana matumaini makubwa ya ushindi katika mchezo huo kutokana na maandalizi mazuri aliyoyafanya kocha wao Mkongoman, Mwinyi Zahera.

 

“Tunajua wapinzani wetu Alliance watakuwa nyumbani wakiwa na sapoti kubwa ya mashabiki, lakini hiyo haitufanyi sisi tupoteze mchezo huo ambao tunahi­taji pointi tatu muhimu.

 

“Alliance siyo timu nyepe­si, ni timu nzuri lakini hiyo haitufanyi sisi tuogope, zaidi tutaingia uwanjani kwa ajili ya ushindi kutokana na umuhimu mkubwa wa mchezo huo.

 

“Hivyo, kama wachezaji tayari tumeshika maelekezo na mbinu

ambazo kocha wetu ametupa­tia kwa ajili ya kupata ushindi ambacho ndiyo kitu muhimu kwetu,” alisema Ajibu.

Stori na Wilbert Molandi, Championi Ijumaa

Comments are closed.