The House of Favourite Newspapers

Zahera amalizana na straika Mzimbabwe

Jacques Tuyisenge

KOCHA wa Yanga Mwinyi Zahera amesema kuwa straika wa FC Lupopo, Rodrick Mutuma raia wa Zimbabwe amekubali kutua Jangwani.

 

Zahera amekuwa akifanya usajili wa chinichini lakini kwa kasi ya hali ya juu huku ikielezwa kuwa anakaribia kumnasa mshambuliaji wa Gor Mahia Jacques Tuyisenge, Eric Rutanga wa Rayon Sports na Hamimu Abdulkarim wa APR ya Rwanda. Tayari imebainika kuwa

 

Kocha huyo amemsajili mlinda mlango wa Bandari FC ya Kenya, Farouk Shikalo ambaye ndiye kipa bora kwa sasa nchini humo.

Mwinyi Zahera

Chanzo chetu makini kimelieleza Championi Jumatano kuwa, Zahera amekuwa akizungumza na Mutuma kwa muda mrefu na wamefikia pazuri na muda wowote atampa advansi sambamba na wachezaji hao wa Rwanda.

 

“Amekuwa akitueleza kwa muda mrefu sana juu ya mazungumzo yake na Mutuma, ambapo mambo yalikuwa hayaendi anavyotaka kutokana na klabu yake ya Lupopo kuonyesha nia ya kutomuachia.

 

“Lakini juzi amesema kuwa ameshazungumza naye na mambo yote yanakwenda vizuri na atakuja Yanga,”kilisema chanzo chetu cha kuaminika ndani ya Yanga.

 

Championi baada ya kupata taarifa hizo lilimtafuta Zahera mwenyewe akasema; “Niko kwenye mazungumzo na wachezaji wengi tu na wala siyo hao unaonitajia pekee, ila kujua ni nani ataungana nasi msimu ujao hilo nitaliweka wazi mara baada ya ligi kumalizika na nitakapokamilisha usajili.”

 

“Kuna mambo mengi bado yanahitajika ndani ya klabu, lakini elewa kuwa wengi nimeongea nao.

 

“Nafahamu watu wengi wana kiu ya kujua nini tutakifanya hivyo, sipo tayari kuweka hadharani mambo yangu ya usajili kwani bado nina angalia wachezaji hapa ndani na huko nje,” alisema Zahera

Stori Musa Mateja Dar es Salaam

Comments are closed.