The House of Favourite Newspapers

Viongozi wapya wasogeze nusu fainali ya Yanga

MCHEZO wa Nusu Fainali wa Kombe la Shirikisho kati ya Lipuli FC dhidi ya Yanga utapigwa Mei 6, mwaka huu ili kupisha Uchaguzi Mkuu wa Yanga.

Awali, uchaguzi na mchezo huo ulipangwa uchezwe Mei 5, mwaka huu unaotarajiwa kupigwa kwenye Uwanja wa Samora huko Mkoani Iringa.

 

Mchezo huo unatarajiwa kujaa upinzani kutokana na Yanga kuwa na hasira za kupoteza mchezo wao wa ligi uliopita ambao walifungwa uwanjani hapo bao 1-0. Akizungumza na Championi Jumatano, Mratibu wa timu hiyo,

Hafidh Saleh alisema kuwa tayari wamepokea taarifa ya kusogezwa mbele mchezo kutoka TFF. Saleh alisema, ilikuwa ni ngumu kufanya uchaguzi siku ya mechi muhimu ya nusu fainali ambayo viongozi akili zao zitakuwa kwenye uchaguzi utakaowapa viongozi wapya wa kuiongoza Yanga.

 

“Mchezo wa Nusu Fainali dhidi ya Lipuli hautachezwa tena Mei 5 na badala yake utapigwa Mei 6, mwaka huu baada ya TFF kuusogeza mbele mchezo huo,”alisema

Comments are closed.