The House of Favourite Newspapers

Man U sasa hakukaliki, Bosi mkubwa amuweka kiti moto Ole

Ed Woodward

MKURUGENZI Mtendaji wa Klabu ya Manchester United, Ed Woodward amelazimika kufika kwenye mazoezi ya timu hiyo na kufanya mazungumzo na Kocha Ole Gunnar Solskjaer pamoja na msaidizi wake, Mike Phelan baada ya kuona mwendelezo mbovu wa timu hiyo.

 

Bosi huyo alifika kwenye mazoezi ya juzi Alhamisi ikiwa ni siku moja tangu timu hiyo ilipofungwa mabao 2-0 na wapinzani wao kutoka katika jiji moja, Man City.

Woodward aliwasili mida ya mchana kwenye viwanja vya mazoezi vya Carrington kuzungumzia vipigo saba katika mechi tisa zilizopita kiasi cha kuifanya timu hiyo kuwa katika nafasi mbaya ya kukosa michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ikiwa haitashika nafasi nne za juu katika msimamo wa ligi kuu.

 

Kipigo cha mabao 2-0 kimeivuruga United na kumekuwa na bidii inafanyika kuhakikisha hali inarejea kwenye mstari ili kuokoa jahazi.

 

Kiungo Paul Pogba inadaiwa kuwa alitoa hotuba fupi kwenye vyumba vya kubadilishia nguo wakati wa mchezo dhidi ya Man City lakini hiyo haikusaidia kuwaokoa na kipigo walichokipata.

 

Matokeo hayo mabaya klabuni hapo ni ya kwanza kutokea baada ya kupita miaka mingi, yameongeza presha kuwa huku taarifa kuwa Pogba anatarajiwa kuondoka klabuni hapo kwenda Real Madrid zikizidi kuwavuruga.

 

Man United imesisitiza kuwa Pogba hatauzwa lakini taarifa za ndani zinaeleza kuwa klabu hiyo ipo tayari kumuuza mchezaji huyo hasa baada ya kuwepo taarifa kuwa Madrid wapo tayari kumtoa Gareth Bale kama sehemu ya usajili huo. Upande mwingine, kipa wa timu hiyo, David de Gea naye ameendelea kuiweka katika presha klabu yake kutokana na kutokuwa na uhakika wa nini ambacho kitatokea mwishoni mwa msimu huu.

 

Imeelezwa kuwa De Gea alikuwa anakaribia kumwaga machozi mara baada ya mchezo dhidi ya Man City huku akionekana kuwa mpole katika mazoezi yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Carrington, juzi, hiyo ni kutokana na kuonekana kama amehusika katika kuifungisha timu hiyo.

 

United inataka kubaki na kipa huyo ambaye anahusishwa kwenda Paris SaintGermain, hajasaini mkataba mpya hadi sasa na kuna taarifa kuwa kuna baadhi ya mambo hayapo sawa katika suala lake la kuelekea mkataba mpya. Straika wa timu hiyo, Romelu Lukaku naye ni mmoja wa wanaoaminika kuwa wataondoka, ameshindwa kuwa na ubora mzuri na hata katika mchezo uliopita alianzia benchi.

 

Raia huyo wa Ubelgiji alinukuliwa akisema kuwa ana ndoto ya kucheza soka Italia, imeelezwa wakala wake, Federico Pastorello ameshaanza kuzungumza na klabu kadhaa za Serie A. Ili kuruhusu aondoke, United inahitaji kurejesha sehemu ya dau lake kubwa ambalo ilitumia kumsajili staa huyo, alisajiliwa kwa pauni 75m na analipwa pauni 250,000 kwa wiki.

 

Mahitaji binafsi nayo yanaweza kuwa kikwazo kumruhusu Alexis Sanchez kuondoka
kutokana na kushindwa kucheza katika ubora na kukosa namba katika kikosi cha kwanza. Staa huyo amecheza kwa dakika 17 ndani ya mwezi wote uliopita kutokana na kuwa majeruhi.

 

Mshahara wake wa pauni 500,000 kwa wiki ni kikwazo kwa timu nyingi kumsajili licha ya kuwa Ole ameonyesha nia ya kuwa tayari kumruhusu kuondoka.

Wachezaji wengine waliokaa mguu sawa kuondoka klabuni hapo mwezi ujao ambapo msimu utakuwa ukikamilika ni Ander Herrera, Juan Mata, Antonio Valencia na Matteo Darmian.

EXCLUSIVE: SAMATTA Azuiwa Kuoa BABA Yake Afunguka KISA!!

Comments are closed.