RAIS WA SHIRIKISHO LA MISRI AMPIGA CHINI KOCHA MKUU KISHA NAYE ABWAGA MANYANGA

BAADA ya timu ya Taifa ya Misri kutolewa hatua ya 16 bora na timu ya Afrika Kusini kwa kufungwa bao 1-0 jana uwanja wa Taifa wa Cairo, imeripotiwa kuwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Misri, Hany Abourida amemtimua kocha Mkuu Javier Aguirre.

Aguirre alikuwa na kandarasi ya miaka minne ndani ya kikosi cha Mapharaoh hao na alikuwa analipwa dola 120,000 kwa mwezi, pia imeripotiwa kwamba baada ya kutoa adhabu hiyo Rais huyo amejiuzulu nafasi yake pamoja na makamu wake naye Ahmed Shobeir naye amejiuzulu.

Loading...

Toa comment