Waziri Shonza Amfagilia Ally Rehmtullah Kwa Vazi La Kitenge

Naibu wa Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Mhe. Juliana Shonza akiongea.

MBUNIFU mkongwe nchini Ally Rehmtullah ametikisa katika maonesho ya vazi la kitenge katika kiwanja cha Mashujaa Mnazi mmoja ambapo alikuwa akisherehekea pia miaka 12 tangu ameingia katika sanaa ya ubunifu wa mavazi.

Tukio hilo ambalo limefanyika jana, mgeni rasmi alikuwa Naibu wa Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Mhe. Juliana Shonza ambaye amempongeza Ally kwa kazi kubwa ambayo anaifanya katika tasnia ya ubunifu.

“Nampongeza sana Ally Rehmtullah kwa sababu ni mdau anayefanya vizuri katika sanaa ya ubunifu wa mitindo na tumezoea kumuona akibuni mavazi mbalimbali lakini kwa sasa amekuja tofauti, ametuonyesha vazi la kitenge na kwa kutumia fursa hii vijana watapata ajira kwa sababu kitenge kilikuwa hakithaminiwi lakini tumeona kwa sasa watu wengi wameingia kwenye vazi hilo linapendwa na wengi hivyo, mafundi cherehani watapata ajira na pia hii kampuni ya Hightech Wear itatusaidia kuitangaza nchi yetu pia hasa katika uchumi wa viwanda,”alisema Waziri Shonza.

Ally Rehmtullah

Katika siku hiyo, wanamitindo mbalimbali walipanda jukwaani na kuonesha mavazi mengi ya vitenge na mwisho kabisa Ally Rehmtullah naye alipanda kuonesha vazi lake na kuibua shangwe kwa wahudhuriaji wengi waliofika hapo.

Imeandaliwa na Neema Adrian/ GPL

RC MWANRI Alivyo KANYAGA Mbele ya DIAMOND, Watu HOI Ukumbini!!


Loading...

Toa comment