The House of Favourite Newspapers

TANZIA: MENEJA WA SHIRIKA LA AGPAHI AGNES KABIGI AFARIKI DUNIA

Marehemu Agnes Kabigi enzi za uhai wake.

Meneja Mawasiliano wa asasi inayolenga kutokomeza UKIMWI kwa watoto na familia Ariel Glaser Pediatric AIDS Healthcare Initiative (AGPAHI), Bi. Agnes Kabigi amefariki dunia leo Ijumaa Julai 26,2019.

 

Taarifa za awali zinasema Agnes Kabigi ambaye ni mwandishi wa habari wa muda mrefu amefariki dunia baada ya kuanguka ghafla wakati akitekeleza majukumu yake wilayani Kahama mkoani Shinyanga.

 

Taarifa kifo cha Agnes Kabigi zimethibitishwa na Mkurugenzi wa Shirika la AGPAHI, Dkt. Sekela Mwakyusa.

“Ni kweli ndugu yetu Agnes Kabigi ametutoka,amefariki dunia huko Kahama baada ya kuanguka akiwa kwenye majukumu ya kikazi” – Dkt. Mwakyusa.

Comments are closed.