The House of Favourite Newspapers

Mwanafunzi Amkana Mwalimu Aliyedaiwa Kumpa Mimba

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Kigoma imemwachia huru Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Nyantore iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma baada ya upande wa mashtaka kuomba kutoendelea na shauri hilo kufuatia shahidi wa pili, mwanafunzi mwenye mimba, kueleza mbele ya mahakama kuwa hamfahamu mtu aliyeshiriki naye mapenzi hadi kupata mimba.

 

Aidha shahidi huyo amekana kuwa na umri wa miaka 16 kama upande wa mashtaka ulivyosema kupitia upelelezi wa polisi na kwa mujibu wa baba wa mwanafunzi huyo amesema binti yake ana umri wa miaka 19 na kwa muda mrefu polisi walikuwa wakimshawishi aseme ana miaka 16 tofauti na anavyofahamu.

Comments are closed.