The House of Favourite Newspapers

Dereva bodaboda anusurika kichapo mikocheni Dar

0

Baadhi ya wananchi wakishudia bodaboada hizo zikiwa chini baada ya tukio husika.

2.Bodaboda iliyopo kwa mbele ni ambayo ilikuwa ikikimbizwa na aliyekuwa akituhumu kuibiwa.Bodaboda iliyo mbele ni ambayo ilikuwa ikiendeshwa na aliyekuwa akituhumu kuibiwa.

3.Bodaboda iliyotuhumiwa kumpakiza mwanamke huyo ambayo walianguka nayo na kupasuka kichwa baada ya kugonga mti kwa mbele.

Bodaboda iliyotuhumiwa kumpakiza mwanamke huyo ambayo walianguka nayo na kupasuka kichwa baada ya kugonga mti kwa mbele.

4.Baadhi ya watu wakishudia tukio hilo.Baadhi ya watu wakishudia tukio hilo.

5.Almanusura wa tukio hilo aliyekuwa akikimbizwa. ‘Manusurina’ wa tukio hilo aliyekuwa akikimbizwa.

DEREVA mmoja wa bodaboda aliyejitambulisha kwa jina moja tu la Gifti amenusurika kichapo mara baada ya kutuhumiwa kuwa mwizi kwa kukwapua mkoba wa mwanamama mmoja ambaye hakujulikana jina.
Tukio hilo limetokea maeneo ya Mikocheni jijini Dar mapema hii leo, ambapo mashuhuda wa tukio hilo wamesema kuwa ‘manusurina’ huyo alikuwa akitokea maeneo ya Sayansi barabara inayopita maeneo ya (Rose Garden ) ambapo dereva huyo alikuwa akifukuzwa kwa nyuma na bodaboda mwingine aliyekuwa amempakiza mwanamama aliyedaiwa kuibiwa mkoba.
Wamesema kuwa dereva huyo alikuwa akimfukuzia kwa nyuma lakini alimpita kwa mbele akamgonga na kuanguka mtaroni huku mama huyo aliyekuwa amepakizwa akipiga kelele za mwizi…mwizi..mwizi ambapo watu walifika kutaka kujua nini kisa chake.
Mmoja wa mashuhuda aliyejitambulisha kwa jina la Shukuru ameelezea tukio hilo akisema kuwa dereva ambaye alikuwa amempakiza mwanamke huyo mara baada ya kuanguka mtaroni alijingonga kwenye mti kichwani ambapo aliumia sana na alikuwa hawezi hata kuongea badala yake alikimbizwa hospitalini.
Amesema mwanamke huyo alipohojiwa kisa cha kutamka maneno hayo ya mwizi..mwizi, lengo lake lilikuwa ni kutaka asimame maana alikuwa akimkimbiza ili aweze kusimama kutokana na kugonga gari lake na kukimbia.
Shuhuda huyo alisema kabla hawajaanza kumrushia kichapo njemba huyo waliamua kupata maelezo ya mama huyo baada ya kujiridhisha waliamua kumwachia kutokana na kisa cha tukio husika kuhusisha masuala ya usalama wa barabarani.
Mwandishi wetu alifika eneo la tukio na kukuta tayari mwanamke huyo na dereva wake wakiwa tayari wamekwishaondoka eneo husika na kumkuta dereva tu aliyekuwa akituhumiwa kupora akigalagala pembeni mwa barabara.

HABARI NA DENIS MTIMA/GPL

Leave A Reply