The House of Favourite Newspapers

Wateja wa NMB sasa kupata mikopo ndani ya siku nne

0

1

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB Plc, Ineke Bussemaker akizungumza na waandishi wa Habari kuhusu mfumo wa kisasa wa utunzaji wa taarifa za mikopo uliozinduliwa na Benki hiyo. Mfumo huo utatutumika kwenye kanzi data ya Mikopo ya Benki hiyo (CRB’s) kwa lengo la kuwawezesha wateja wakubwa na wadogo wa wanaoomba mikopo kuipata ndani ya siku 1 hadi 4.

2

Ofisa Mkuu Udhibiti wa Hasara wa Benki ya NMB, Tom Borghols (wa pili kutoka kushoto) akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa Habari (hawapo pichani) namna Benki ya NMB inavyoongoza katika utoaji wa mikopo nafuu kwa makundi mbalimbali.

3

Kaimu Mkurugenzi wa Wateja Wadogo wa Benki ya NMB – Abbdulmajid Nsekela (kulia) akitoa ufafanuzi kuhusu kuanzishwa kwa mfumo wa kisasa wa utunzaji wa taarifa za mikopo kwa wateja uliozinduliwa na Benki ya NMB na jinsi utakavyoongeza ufanisi kwa kuwawezesha wateja kupata mikopo kwa haraka. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa NMB Plc – Ineke Bussemaker.

4 IMG_9132
Wanahabari wakichukua matukio katika eneo hilo.

Wateja wa NMB sasa kupata mikopo ndani ya siku nne

Benki ya NMB imezindua mfumo wa kisasa wa kuhifadhi taarifa za wateja utakaotumika kwenye kahifadhi taarifa ya Mikopo ya Benki hiyo ( CRB’s) kwa lengo la kuwawezesha wateja wakubwa na wadogo wanaoomba mikopo kuipata ndani ya siku 1 hadi 4 tofauti na ilivyokuwa mwanzo kutokana na taarifa zao kupatikana kiurahisi kwa mfumo wa kielektronik.

Kwa mfumo huo na kwa kutumia mfumo ujulikanao kama Simbuka Benki ya NMB itaweza kufuatia taarifa za wateja kwa ukaribu zaidi. Mfumo huu ni Kiama kwa wakopaji ambao siyo waaminifu na wanaokopa benki zaidi ya moja na kuzidisha Kiwango kilichowekwa.

Mfumo huo ni mahususi kwa waombaji wa mikopo ya wafanyakazi (Salaried Workers Loans) na mikopo ya wajasiliamali mbalimbali.

Mfumo huo uliojengwa kwa ushirikiano na wataalam kutoka nchini Uholanzi kutoka kampuni la Simbuka, unawezesha ushirikiano wa taarifa za kibenki kutoka benki moja kwenda nyingine na sasa wateja watapata mikopo yao ndani ya siku 4 kutokana na taarifa za mifumo kuwasiliana kwa haraka sana.

Aidha, amesema mabadiliko hayo yaliyoanzishwa na Benki Kuu ya Tanzania (BOT) yamechukuliwa kwa umakini na Benki hiyo kutokana na idadi kubwa ya mikopo na wateja inaowahudumia. NMB huhudumia maombi ya mikopo zaidi ya 700 kwa siku.

Mtandao huo utasaidia Benki ya NMB kufuatilia na kubainisha mwenendo wa wateja wanaolipa vizuri na vibaya.

Leave A Reply