The House of Favourite Newspapers

MWANAHARAKATI WA MAUAJI YA TEMBO AUAWA

0
MWANAHARAKATI WA MAUAJI YA TEMBO
Mwanaharakati wa kuhifadhi wanyama pori Wayne Lotter, enzi za uhai wake.

MWANAHARAKATI wa kuhifadhi Wanyamapori raia wa Afrika Kusini, Wayne Lotter, amepigwa risasi na kuuawa maeneo ya nyumbani kwake, Masaki jijini Dar.

 

Lotter alikuwa mwanzilishi wa PAMS Foundation, shirika ambalo limekuwa katika mstari wa mbele kusaidia kupambana na uwindaji haramu na biashara ya pembe za ndovu nchini. Polisi jijini Dar es Salaam wanasema wanachunguza waliotekeleza mauaji hayo, wakati huu ikiwa bado haijafahamika ni kwa nini aliuawa na waliohusika.

 

Waliofanya kazi na mwanaharakati wa mauaji ya tembo Lotter akiwemo Jane Goodall, raia kutoka Uingereza na Michel Lanfrey raia wa Ufaransa wamemwelezea mwanaharakati huyo kama shujaa aliyefanya kazi kwa bidii kuhakikisha kuwa uwindaji haramu unapungua nchini.

 

Inadaiwa kuwa, kabla ya kuuawa kwake, alikuwa amepokea vitisho kuhusu kazi yake lakini pia upinzani mkali kuhusu jitihada zake za kuzuia uwindaji haramu. Shirika la PAMS International linaifadhili Serikali ya Tanzania kupitia taasisi maalum ya kufanya uchunguzi na kuwakamata wawindaji haramu na takwimu zinaeleza kuwa wawindaji karibu 900 wametiwa mbaroni.

STORI: ALLY KATALAMBULA| RISASI JUMAMOSI

Leave A Reply