The House of Favourite Newspapers

Buswita Akabidhiwa Namba Ya Chirwa

Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Pius Busitwa.

KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Pius Busitwa, leo atacheza namba tisa akimrithi mshambuliaji Mzambia, Obrey Chirwa aliyeshindwa kuongozana na msafara huo kuelekea Shelisheli.

 

Kutokana na ushindi wa bao 1-0 Jijini Dar es Salaam, Yanga leo ina­hitaji suluhu, sare, ushindi na hata ikifungwa mabao 2-1 itasonga mbele kwenye hatua ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

 

Mzambia huyo aliachwa katika msafara huo kwa kile kilichodaiwa kupata maumivu ya misuli ingawa habari zingine zinadai kwamba hayuko sawa na viongozi.

 

Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Championi Jumatano kutoka ndani ya benchi la ufundi la timu hiyo, Kocha Mkuu Mzambia, George Lwandamina, ameanza kumuandaa Buswita kucheza nafasi hiyo katika mazoezi ya siku ya kwanza tangu wamefika nchini

 

Kwa mujibu wa programu za mazoezi ya Lwandamina, Buswita amekuwa akicheza nafasi hiyo ya ushambuliaji wa kati namba tisa, nyuma yake namba kumi atacheza Ibrahim Ajibu tangu Yanga ilipoanza programu mjini hapa.

 

Awali Buswita alikuwa aki­tumika kama namba saba la­kini benchi la ufundi limean­galia na kujiridhisha kwamba ndiye mchezaji pekee anayeweza kuongeza kasi ya mashambulizi ndio maana wakamhamisha.

 

Katika mazoezi yaliyofan­yika mchezaji huyo alionyesha uw­ezo mkubwa kwenye kupachika mabao na kutengeneza na­fasi ambazo zinamfaa sana Ajibu haswa kwa aina ya matokeo Yanga inayosaka leo Jumatano.

 

Meneja mkuu wa timu hiyo, Hafidh Saleh alipoulizwa kuhusu hilo ali­sisitiza kuwa; “Kocha anawaandaa baadhi ya wachezaji watakao­chukua nafasi ya Chirwa kucheza nafasi yake na kati ya hao yupo Buswita. Tangu tumefika hapa Shelisheli katika mazoezi yake ko­cha wetu Lwandamina amekuwa akimpanga Buswita kucheza nam­ba tisa na chini yake namba kumi anacheza Ajibu, hivyo ninaamini wachezaji hao watacheza pamoja katika nafasi hiyo.”

Hafidh ambaye ni miongoni mwa wanachama waandamizi wenye heshima kubwa ndani ya Yanga, aliongeza kwamba kwa hali iliyo lazima washinde mchezo huo bila wasiwasi.

Comments are closed.