The House of Favourite Newspapers

BREAKING: MBOWE AISHUTUMU NEC, JESHI LA POLISI

 

MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe ameishutumu Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuwa walishindwa kuwasikiliza ikiwemo kuwapa fomu mapema ambazo zingewawezesha mawakala wao kuingia kwenye vituo vya uchaguzi na kufanya majukumu yao, jambo ambalo lilisababisha mtafaruku katika baadhi ya vituo hivyo wakati wa uchaguzi mdogo wa Feb. 17,.

 

Mbowe amesema hayo leo Feb 27, 2018 wakati akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam na kudai kuwa Jeshi la Polisi limekuwa likitumia nguvu kuwadhibiti vyama vya wapinzani.

 

‘Tuliandamana kwenda kwa msimamizi mkuu wa uchaguzi Kinondoni kutaka vyeti vyetu ili mawakala wetu waingie vituo vya kura, polisi walitumia risasi za moto kututawanya. Binti Akwilina aliuawa, wengine watano walijeruhiwa kwa risasi.

“Hadi sasa Jeshi la Polisi linawashikilia vijana waliopigwa risasi na hawajafikishwa Mahahakani wala kuhudumiwa. Tunafahamu wanawanyima dhamana wahanga hao ili kuficha majeraha na maumivu, wanajua wakiwaachia waandishi mtawaona na mtawahoji hii,  si Tanzania tunayoijua.

 

“Tumewaelekeza mawakili wetu wa Chadema wapeleke maombi kwa ajili ya watuhumiwa wanaowashikilia kwa maandamano na wengine waliojeruhiwa kwa risasi, wafikishwe mahakamani ili wapatiwe dhamana.

“Leo nitaongoza viongozi wenzangu wa Chadema kuitikia wito wa polisi, lakini Katibu Mkuu, Dkt. Mashinji hatojumuika na sisi kwa kuwa yupo nje ya nchi kikazi. Tutaheshimu sheria na katiba ya nchi lakini hatutamuogopa mtu,” alisisitiza Mbowe.

 

Akizungumzia matukio ya mauaji ambayo yamekuwa yakitokea hapa nchini, Mbowe amesema:

 

“Mauaji yanayotokea hapa nchini, Serikali inapotosha kwa kusema wanaofanya unyama huo hawajulikani, ni dhahiri mauaji hayo Serikali inajua wanaofanya ukatili huu ni akina nani. Mkoa wa Morogoro ndiyo unaongoza kwa kuwabambikizia kesi viongozi wetu wa Chadema hata kwa mauaji, munaongoza kwa kuwa kuna historia ya watu wetu wa Chadema kuuawa mkoani humo.

 

“Imefikia wakati tumeanza kuzoea kuuana, tumeanza kuzoea vifo. Jambo hili si la kushabikia, ni hatari kwa taifa letu, lazima tuchukue hatua. Haya mambo hayakuwepo mwanzoni.”

Mbowe ameenda mbali zaidi na kumjibu Wakili Cyprian Msiba aliyedai hivi karibuni kuwa Chadema kimepeleka vijana nje ya nchi kupata mafunzo.

 

“Yupo mtu anaitwa Musiba, anasema Chadema imepeleka zaidi ya vijana 5,000 kwenda kusoma Ujerumani, sisi hatujasomesha watu. Anamtaja Yericko Nyerere ambaye hajawahi kuwa hata mtendaji wa chama, ni Mtanzania mwenye mapenzi na nchi yake Hizi chaguzi zote zitaendelea kuzaa maumivu kama hatua ‘seriou’s hazitachukuliwa katika nchi hii,” alisema Mbowe.

VIDEO: MSIKIE MBOWE AKIZINGUMZA HAPA

Comments are closed.