The House of Favourite Newspapers

MSHANGAO NYUMBANI KWA LISSU

WAKATI Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu ‘akiwachimba biti’ waliompiga risasi na kumuacha na kilema, mshangao umeibuka nyumbani kwake Tegeta jijini Dar kutokana na mazingira ya ukimya yaliyopo huku ikidaiwa kuwa hakuna anayeishi ndani ya mjengo huo.

 

Inadaiwa kuwa, Lissu ambaye anaendelea kufanyiwa matibabu nchini Ubelgiji ameichukua familia yake yote na kuishi nayo huko ili kuyaacha maisha mengine yaendelee hata kabla ya kurudi Bongo.

Mmoja wa majirani wa kiongozi huyo aliyeomba hifadhi ya jina lake aliliambia Uwazi kuwa, amekuwa akishangazwa na mazingira ya sasa ya nyumbani hapo huku akidai kuwa hakuna anayeishi hapo kwa sasa na nyasi zimechukua nafasi.

 

“Hapa nyumbani kwa Lissu sasa hivi panatushangaza kwa kweli, zamani kuna kijana tulikuwa tunamuona hapa lakini sasa hivi pamekuwa kimya, inavyoonekana nyumba imekimbiwa na mwenyewe kila siku tunasikia anarudi… anarudi lakini mpaka leo jiii,” alisema jirani huyo na kuongeza:Related image

“Kuna siku nilitamani sana kujua Lissu anaendeleaje na anarudi lini, nikaenda pale nyumbani kwake, nimegonga weee, sikufunguliwa geti, kesho yake tena nikaenda lakini sikufanikiwa kuona mtu yeyote sasa nashindwa kuelewa nini kinaendelea, kwamba kuna mtu lakini anaishi kwa machale au nyumba imekimbiwa, naombeni kama mna namba ya yule kaka yake aliyeko Singida mnipatie.”

 

Kufuatia maelezo hayo, hivi karibuni makamanda wa Kikosi cha Oparesheni Fichua Maovu (OFM) kilitinga nyumbani kwa Lissu saa 2 asubuhi na kuweka kambi kwa takribani saa 6. Baada ya kufika nyumbani hapo, mmoja wa makamanda alilisogelea geti na kugonga sana lakini hakuna aliyetoa ushirikiano huku ndani kukionekana kumetulia tuliii. Kufuatia ukimya huo, makamanda hao walilazimika kuongea na majirani ambao nao walikuwa na sintofahamu kuhusu mazingira ya nyumba hiyo.

 

“Sasa hivi hakuna anayeishi hapo, nawaonaga vijana watatu ambao wanakuja wanafanya usafi na kuondoka ila kuna huyo mmoja ambaye anabaki hapa anaitwa Burali ndiyo mara nyingi namuonaga anashinda hapa, sijui kama analala au laa,” alidai mzee mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Johnson ‘Baba Fred’.

Mwingine anayefanya biashara zake za duka karibu na nyumba ya Lissu alisema: “Hiyo nyumba kila siku ipo hivyohivyo kama mnavyoiona, ipo kimyaa tu ndiyo maana hata nyinyi mmegonga sana hakuna mtu aliyekuja kuwafungulia, yaani tangu yule mzee aende kutibiwa Ubelgiji pamekuwa kimya sana hakuna hata ndugu zake wanaoishi humo au hata kuja mara mojamoja kama ilivyokuwa mwanzo kipindi mwenyewe yupo, sijui wanaogopa au vipi.

 

“Kuna vijana wanafikaga hapa, wanakuwa wanyonge sana kama wanaoomboleza, hawana hata raha ya kukaa ndiyo maana mara nyingi wanafanyafanya usafi na kuondoka sidhani kama wanalalaga hapo.”

Hata hivyo, baada ya makamanda hao kukaa eneo hilo kwa takribani saa 6 bila kuona mtu yeyote akitoka ama kuingia kwenye nyumba hiyo, waliamua kuondoka na kwenda kuendelea na majukumu mengine.

STORI: SHAMUMA AWADHI NA NEEMA ADRIAN

Comments are closed.