The House of Favourite Newspapers

Azam FC yamkomalia Nyosso mahakamani

0

LICHA ya kupewa adhabu na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), uongozi wa Azam FC umepanga kumchukulia hatua nyingine za kisheria nahodha wa Mbeya City, Juma Nyosso.

Azam imesema inakomaa kwa kuwa imeguswa jinsi nahodha wake John Bocco alivyodhalilishwa na Nyosso hivyo lazima wamchukulie hatua mchezaji huyo nje ya uwanja.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam, Saad Kawemba aliliambia Championi Jumamosi kuwa, wamepanga kulihamishia sakata hilo nje ya uwanja kutokana na udhalilishaji alioufanya Nyosso.

Kawemba alisema, “Tunalazimika kufanya hivi kwa kuwa viongozi wa Mbeya City wameshindwa kutoa tamko lolote kutokana na kitendo hicho. Tutakutana na mwanasheria wetu kwa hatua zaidi, hatuwezi kukubali”

Leave A Reply