The House of Favourite Newspapers

Ndege Yalipuka Urusi, 41 Wafariki Dunia – Video

WATU 41 wamefariki dunia baada ya ndege ya Shirika la Ndege la Urusi (Aeroflot) kulipuka moto wakati ikitua kwa dharura katika uwanja wa ndege wa Sheremetyevo mjini Moscow nchini humo.

Video katika mitandao ya kijamii zinaonyesha baadhi ya abiria wakitumia mlango wa dharura na kutoka kwenye ndege hiyo ya Aeroflot iliyokuwa inateketea kwa moto.

Watoto wawili na mhudumu mmoja ni miongoni mwa waliofariki kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Urusi.

Shududa mmoja amesema ilikuwa ni “miujiza” kwamba kuna aliyenusurika mkasa huo wa ndege iliyokuwa imebeba abiria 73 na maofisa watano wa ndege.

 

“Watu 37 wamenusurika ambao ni abiria 33 na maofisa wanne wa ndege hiyo,” amesema ofisa wa Kamati ya Uchunguzi, Yelena Markovskaya.

Aeroflot limesema ndege hiyo ililazimika kurudi katika uwanja wa ndege ” kutokana na sababu za kiufundi”, lakini halikufafanua zaidi.

Ndege hiyo aina ya Sukhoi Superjet-100, iliondoka uwanja wa ndege wa Sheremetyevo majira ya saa 18:02 kwa saa ya huko kutoka eneo la Murmansk.

Taarifa zinasema maofisa wa ndege walitoa tahadhari ya wasiwasi wakati kutokana na ” hitilafu” muda mfupi baada ya ndege kuondoka.

 

Baada ya kutua kwa dharura katika uwanja huo wa ndege, injini zake ziliwaka moto,  Aeroflot limesema katika taarifa.

Kaimu Gavana wa mji eneo hilo la Murmansk, Andrey Chibis,  amesema familia za waliofariki katika mkasa huo zitalipwa Dola 15,300 kila moja, huku waathirikwa watatibiwa na watapewa  Dola 7,650 kila mmoja.

Comments are closed.