The House of Favourite Newspapers

Nisamehe Latifa-48

0

ILIPOISHIA WIKI ILIYOPITA

Hapo ndipo mzee Deo alipoanza kusimulia kila kitu kilichotokea katika maisha yake, tangu siku alipokutana na Nahra na mpaka alipompa mimba na wazazi wake kumuagizia watu waende kumpiga mkwara asirudiane na msichana huyo kwani wangemuua.

SONGA NAYO…

“Sikumfukuza mama yako kwa kupenda, nilitakiwa nifanye hivyo kwa kuwa nisingefanya hivyo, ningeuawa,” alisema mzee Deo huku akibubujikwa na machozi.

Kukutana na baba yake ilionekana kuwa faraja kubwa, alibaki akiwa amekumbatiana naye kwa zaidi ya dakika mbili. Furaha aliyokuwa nayo moyoni haikuelezeka hata kidogo.

Kilichofuata baada ya hapo ni kuombana msamaha kwa kila kitu kilichotokea kabla, wakaelekea katika kaburi la Nahra, wakaliona, wakalia kisha kuondoka huku ujenzi wa kaburi hilo ukitakiwa kufanyika haraka iwezekanavyo.

Maisha mapya yakaanza. Kama shukrani ya kumtunza baba yake, Latifa akaamua kumgawia Ibrahim dola laki moja, zaidi ya milioni mia mbili kisha kurudi nchini Marekani tena huku akiwa ameongozana na baba yake kuanza maisha mapya nchini humo ambapo huko angepewa matibabu yote.

Alichokifanya Ibrahim ni kuanza upya, kitu cha kwanza ni kumpa talaka Nusrat kisha kununua nyumba maeneo ya Mbezi Beach na kuanza maisha na mwanamke mwingine aitwaye Zubeda ambaye aliamua kumuoa.

Kwa Latifa, akafanikiwa kufunga ndoa ya kisheria na Dominick nchini Marekani na kuanza maisha ya mume na mke ambapo baada ya mwaka mmoja, wakafanikiwa kumpata mtoto wa kiume na kumpa jina la Angel yaani likiwa na maana ya Malaika.

Kila kitu kikabadilika, maisha ya kimas                                kini aliyoishi kipindi cha nyuma, yakasahaulika, kipindi hicho, aliishi maisha aliyotaka, kwenda alipotaka na kufanya alichotaka. Jina lake likazidi kukua, akajulikana kila kona na baada ya miaka mitatu, akaanza kufanya mchakato wa kutengeneza dawa ya Ugonjwa hatari wa UKIMWI.

MWISHO.

Leave A Reply