The House of Favourite Newspapers

Niyonzima afunga ndoa, kuikosa Azam

0

Martha Mboma, Dar es Salaam

KIUNGO wa Yanga, Haruna Niyonzima, amefunga ndoa ya serikali na mzazi mwenzake Uwineza Nailah juzi Alhamisi mjini Kigali, Rwanda, hivyo hatacheza leo dhidi ya Azam FC.

Ndoa hiyo imefungwa baada ya Niyonzima kutoka kuichezea Rwanda mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia 2018 dhidi ya Morocco uliopigwa nchini humo.

Niyonzima amefunga ndoa hiyo na mkewe huyo ambaye wamekuwa pamoja kwa muda mrefu huku wakiwa na watoto watatu, Atka na Atfa ambao ni mapacha na Rahim.

Kutokana na ndoa hiyo, Niyonzima amechelewa kuwasili kambini Yanga, hivyo Kocha Hans van Der Pluijm alisema: “Sitamtumia Niyonzima katika mechi dhidi ya Azam.”

Leave A Reply