Vodacom Yashinda Tuzo 3 za Huduma Bora Kwa Wateja 2023 Zinazotolewa na CICM
Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom, mwishoni mwa wiki imetangazwa kuwa mshindi wa tuzo tatu za huduma bora kwa wateja nchini, zilizoandaliwa na kutolewa na Chartered Institute of Customer Management (CICM) jijini Dar es Salaam.
Kampuni hiyo ilishinda vipengele vya kitengo cha utoaji wa huduma bora kwa wateja (mshindi), mtandao bora wa huduma za mawasiliano na intaneti (mshindi wa pili), na uwajibikaji kwa shughuli za kijamii (mshindi wa pili).