The House of Favourite Newspapers

Busungu ana kadi nyekundu ya Azam

0

Sweetbert Lukonge, Dar es Salaam

STRAIKA wa Yanga, Donald Ngoma, amedai anamkubali sana Malimi Busungu, lakini mwenzake ameweka wazi kuwa ana uhakika wa kusababisha kadi nyekundu kwa mchezaji wa Azam FC leo kwenye Uwanja wa Taifa.

Yanga na Azam zinakutana kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara katika uwanja huo jijini Dar es Salaam, lakini Busungu amesema kwa historia amekuwa akisababisha kadi nyekundu kila anapocheza dhidi ya Azam.

Busungu akiwa Mgambo JKT kabla ya kujiunga na Yanga, msimu wa 20013/14 alisababisha kadi nyekundu kwa Erasto Nyoni aliyemchezea vibaya, pia msimu uliopita Aggrey Morris alipatwa na tukio kama hilo.

Straika huyo aliliambia Championi Jumamosi: “Nina historia kila nikikutana na Azam katika ligi, mchezaji wao anapata kadi nyekundu kwa kunichezea vibaya, natabiri Jumamosi (leo) itatokea hali hiyo.”

Busungu alisema anajua namna mabeki wa Azam wanavyocheza kwa kutumia nguvu kupita kiasi lakini atahakikisha anafanya vizuri mbele yao endapo atapata nafasi ya kucheza.

Wakati huohuo, Busungu alisema; “Nafurahi kucheza pamoja na Ngoma kwani hata yeye ameniambia anapenda kucheza kikosi kimoja na mimi kwa kuwa anavutiwa na uchezaji wangu wa kupambana.”

Leave A Reply