The House of Favourite Newspapers

Nelly Muosha Magari wa Posta-10

0

CARMpenzi msomaji, wiki iliyopita niliishia pale sharobaro Nelly alipoiweka soda yake ya kopo juu ya dirisha bila kujua kama Doreen ambaye wakati huo alikuwa hajiwezi kufuatia kijana huyo kumpandisha joto la mahaba alikuwa dirishani kwa ndani akimwangalia. Je, kilifuatia nini?” Songa mbele na utamu huu…

Baada ya kuchota mchanga kama chepe kumi na kuzirushia eneo aliloelekezwa na Zakayo, Nelly alipozi kisha akajishika kiuno na kujinyoosha, kitendo hicho kilimhuzunisha sana Doreen.
“Jamani huyu kaka anaumia bure tu, ngoja kama ataendelea kuja hapa lazima nifanye mpango wa kumpa sapoti yoyote,” Doreen aliwaza.

Wakati Nelly akiendelea na kazi, Zakayo alifika kumwangalia, alivyomkuta akiwa kasimama akatabasamu na kujisemea moyoni ‘huyu kazi hii haiwezi na sijui kama kesho atakuja.’

Zakayo aliwaza hivyo bila kujua kama Nelly alipanga kufika pale site kila siku kwa vile palikuwa na mtoto mkali Doreen ambaye wao walikuwa wakimwangalia tu kama dada yao.

“Vipi, leo huu mchanga utaisha kweli?” Zakayo alimwuliza Nelly.
Nelly bila kumficha alimwambia kwa siku ile alichoka sana hivyo angemalizia siku iliyofuata, kufuatia kauli hiyo, Zakayo akacheka na kuingia ndani kumweleza fundi Yassin.

“Kwa kuwa ni mwanaume ataweza, si unajua hizi kazi unapoanza siku ya kwanza zinakuwa ngumu!” fundi Yassin alimwambia Zakayo.

Kufuatia kuelezwa hivyo, Zakayo alipinga na kumwambia fundi Yassin kwamba Nelly akimaliza wiki pale site atampatia shilingi elfu kumi, fundi Yassin akaishia kucheka.
Zakayo alipoingia ndani, Nelly alimalizia soda yake kisha akawafuata wenzake waliokuwa ndani na kushangaa jinsi walivyoweka marumaru katika vyumba viwili.
“Da! Nyie mnapiga kazi sana, kazi hii yote mmeifanya leo?” Nelly aliwauliza.

Fundi Yassin amjibu kwamba mbona walifanya kazi kidogo sana siku hiyo, Nelly akabaki akishangaa, fundi Yassin alipomuuliza kama alimaliza kuhamisha mchanga, akacheka sana na kumwambia atamalizia kesho yake.

Kwa kuwa fundi huyo alikuwa anauelewa usharobaro wa Nelly, hakumsema vibaya kwani alijua atazoea taratibu lakini kwa upande wa Zakayo alijisemea moyoni kwamba Nelly hakuwa mfanyakazi, sijui kwa nini hakumpenda kijana wa watu.

Baada ya kufanya kazi hiyo, Nelly hakuendelea tena na kazi ya kuhamisha mchanga hadi wenzake walipomaliza kazi na baada ya kuoga kwenye bafu la nje, fundi Yassin alikwenda kuonana na Doreen ambaye alimpa bahasha iliyokuwa na hela.

Baada ya kukabidhiwa alimpatia Zakayo shilingi 30,000 halikadhalika Haruni kisha akaiweka ile bahasha mfukoni, Nelly hakuwa na wasiwasi kwani alielewa kingeeleweka mbele ya safari.

Hata hivyo, Nelly alipenda kabla ya kuondoka amuone Doreen akawa anaplani kuhakikisha anafanikisha hilo, fundi Yassin alipowaambia waondoke akamwambia alihisi kiu hivyo ngoja akaombe maji ya kunywa.

“Wewe huna lolote, unataka umuone tu Doreen,” fundi Yassin alimwambia Nelly ambaye alicheka sana na kusema:

“Siyo hivyo bro hayo ni mawazo yako tu mbona mimi nina demu wangu mkali kumpita sijui huyo Doreen halafu mimi mtoto wa kishua kama huyo nitampa nini?” Nelly aliwaambia, wote wakacheka.

“Jamani muda unakwenda, hayo maji nitaenda kukununulia mbele ya safari, halafu kumbuka wewe hapa ni mgeni usije ukaleta picha mbaya bure,” fundi Yassin alimwambia Nelly bila kujua kama sharobaro huyo ilibakia kiduchu kula tende tamu za mtoto wa kishua.

“Haya mkubwa nimekuelewa, twendeni jamani,” Nelly aliwaambia.
Baada ya kutoa kauli hiyo, fundi Yassin aliwaambia waondoke wakatoka lakini wakiwa nje fundi Yassin aliyekuwa kamzoea Anne, dada wa kazi, alimwita ili amuage.
Licha ya kumwita Anne, aliitika Doreen ambaye alitoka nje fasta, na kumwuliza fundi; “Fundi ndiyo mnaondoka?”

“Yeah! Kesho tutafika mapema kuendelea na kazi,” fundi Yassin alimwambia Doreen bila kujua msichana huyo alikuwa na furaha moyoni ya kumuona Nelly.
“Hakuna shida, nawatakia safari njema,” Doreen ambaye alikuwa amevaa kama alivyovaa awali aliwaambia.

Baada ya kumuaga msichana huyo, fundi Yassin, Zakayo na Haruni wakatangulia Nelly alibaki nyuma ambapo aligeuka na kumkonyeza Doreen aliyeachia tabasamu pana.
Mafundi hao walipotoka getini walishika njia hadi ilipokuwa barabara kubwa ambapo Haruni ambaye alikuwa akiishi maeneo hayo aliwaaga wenzake kwamba wangekutana siku iliyofuata.

Baada ya kuagana haukupita muda mrefu daladala iliyotokea Kisauke lilifika, wote watatu walipanda, kwa kuwa siti zilikuwa wazi fundi Yassin na Nelly waliketi pamoja.
Kutokana na uchovu wa kazi, wakiwa kwenye daladala hilo hawakuwa na stori nyingi zaidi ya Nelly kuwatupia macho mademu wazuri aliowaona nje na wawili waliokuwemo ndani ya basi.

Walipofika njia panda ya Wazo Hill maarufu kama Kibaoni, Zakayo aliyekuwa akiishia Bunju alimuaga Yassin na Nelly ambapo fundi Yassin alimsisitiza kuwahi kufika kazini siku iliyofuata.

Leave A Reply