The House of Favourite Newspapers

Mugabe Alivyomwokoa Mwinyi Mwaka 1985- Video

RAIS mstaafu wa serikali ya awamu ya pili ya Tanzania, Ali Hassan Mwinyi, amesema kuwa alipoingia madarakani mwaka 1985, alikuta hazina ya Tanzania ikiwa haina kitu (haina pesa).

 

Hali hiyo ya ukata ilitokana na Tanzania kutumia fedha nyingi wakati wa vita vya Kagera (Tanzania dhidi ya Uganda) na Shirika la Fedha Duniani (IMF) kuisusia Tanzania baada ya Mwalimu Nyerere kukataa masharti yao.

 

Mwinyi asema, aliamua kumfuata Mwalimu Nyerere akamuuliza, afanye nini? Nyerere akamwambia “Tanzania ina marafiki kadhaa, ikiwemo nchi ya Zimbabwe na India, nenda kaombe msaada.”

Hayati Robert Mugabe akawa kiongozi wa kwanza kuisaidia Tanzania.

 

 

View this post on Instagram

 

A post shared by Global Publishers (@globalpublishers) on

Comments are closed.