The House of Favourite Newspapers

Video: Globa Habari Jan 19, 2020 | Makamu Wa Rais Azindua Tuzo Za Quran Kimataifa

0


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania imekuwa na Heshima kubwa Duniani katika mashindano mbalimbali ya Quran kutokana na Vijana na Watu wengi kuchukuwa nafasi za juu katika Mashindano hayo kutokana na jitihada kubwa zinazofanywa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya kuhifadhi Quran Tanzania Sheikh Othman Kaporo.

 

Makamu wa Rais amesema Tanzania ni moja ya miongoni mwa Nchi chache Duniani kati ya Nchi zinazopata Nafasi ya kuweza kuandaa Mashindano ya Tuzo za Kimataifa za kuhifadhi Quran Tukufu ikiwa huu ni mwaka wa nne tokea kuanza kwa mashindano hayo hapa Nchini.

 

Mhe. Samia amesema hayo jana Jioni wakati wa Hafla ya Chakula cha jioni kwa ajili ya uzinduzi wa Tuzo ya Kimataifa ya Quran Tukufu kwa mwaka 2020 iliyofanyika katika ukumbi wa Johari Rotana Hotel Jijini Dar es salaam ambapo alikabidhi Shahada za Pongezi kwa baadhi ya Vijana kwa kuhifadhi na kutunukiwa Ijaza ya Quran kwa Riwaya ya Hafsi.

 

Nae Mwenyekiti wa Jumuiya ya kuhifadhi Quran Tanzania Sheikh Othman Ali Kaporo amesema lengo la mashindano hayo ni kuwakusanya vijana na kuwaweka katika misingi ya madili iliyo bora.

Leave A Reply