The House of Favourite Newspapers

Kampuni Ya Madini Ya Twiga Yaundwa Kulinda Rasilimali Za Watanzania (Picha +Video)

0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akishuhudia utiaji saini wa mikataba ya makubaliano ya kuendesha kwa pamoja kapuni ya Twiga ya uchimbaji wa Madini kati ya Serikali ya Tanzania na Kampuni ya Barrick ambapo kwasasa kampuni mpya ya ubia ya Twiga, Serikali itakuwa na hisa ya asilimia 16 .Halfa iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam. Januari 24, 2020.

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli leo Januari 24, 2020 ameshuhudia utiaji saini wa makubaliano ya ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na Kampuni ya Barrick Gold Corporation, makubaliano ambayo yameunda Kampuni ya Twiga Minerals Cooperation Limited.

Rais Magufuli akizungumza katika hafla ya utiaji saini wa mikataba ya makubaliano ya kuendesha kwa pamoja kapuni ya Twiga ya uchimbaji wa Madini kati ya Serikali ya Tanzania na Kampuni ya Barrick ambapo kwasasa kampuni mpya ya ubia ya Twiga, Serikali itakuwa na hisa ya asilimia 16 .Halfa iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.

Mazungumzo hayo yaliyoanza tangu mwaka 2017 hatimaye yamefika mwafaka ambapo imeundwa Kampuni ya Madini ya Twiga kwa Serikali ya Tanzania kuwa na hisa asilimia 16 na kwamba faida itakayopatikana katika kampuni hiyo, zitagawanywa asilimia 50 kwa 50 kwa manufaa ya Kampuni husika ya Twiga.

Waziri wa Madini Mhe. Dotto Biteko akikidhiana mikataba na Rais wa kampuni ya Barrick Dkt. Mark Bristow iliyosainiwa mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika hafla utiaji saini wa mikataba ya makubaliano ya kuendesha kwa pamoja kapuni ya Twiga ya uchimbaji wa Madini kati ya Serikali ya Tanzania na Kampuni ya Barrick ambapo kwasasa kampuni mpya ya ubia ya Twiga, Serikali itakuwa na hisa ya asilimia 16 Ikulu jijini Dar es Salaam.

Akizungumza baada ya utiaji saini wa makubaliano hayo, Rais Magufuli amesema kuwa hiyo ni hatua kubwa kwa Watanzania baada ya mazungumzo hayo kufika mwafaka kuundwa Kampuni hiyo ya Twiga itakayokuwa na manufaa kwa Wananchi wa Tanzania katika rasilimali zao.

Waziri wa Madini Mhe. Dotto Biteko akiwa na Rais wa kampuni ya Barrick Dkt. Mark Bristow wakionyesha Mikataba iliyosainiwa mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika hafla ya utiaji saini wa mikataba ya makubaliano ya kuendesha kwa pamoja kapuni ya Twiga ya uchimbaji wa Madini kati ya Serikali ya Tanzania na Kampuni ya Barrick ambapo kwasasa kampuni mpya ya ubia ya Twiga, Serikali itakuwa na hisa ya asilimia 16 Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais Magufuli amesema huo ni ushindi mkubwa kwa Watanzania kutokana na hapo awali kudanganywa kuhsusu Madini hayo, “Barrick ni Kampuni kubwa duniani kufanya nao mazungumzo sio jambo dogo mwanzo Madini yalipokuwa yanachukuliwa Watanzania tuliamini ni mchanga, tunajiuliza swali kama ni mchanga kwa nini usafirishwe hadi nje ya nchi? baadae tulielewa kwamba ule haukuwa mchanga”, amesema Rais Magufuli.

Mikataba iliyosainiwa

Mikataba iliyosainiwa ni mkataba wa msingi wa makubaliano, menejimenti na utoaji huduma, mkataba wa wanahisa wa kampuni ya Twiga, mkataba wa wanahisa wa North Mara.

Mingine ni mkataba wa wanahisa wa Bulyankuru, mkataba wa wanahisa wa Buzwagi, mkataba wa maendeleo ya mgodi wa North Mara, mkataba wa maendeleo ya mgodi wa Bulyanhulu na mkataba wa maendeleo wa mgodi wa Pangea.

Aidha katika hafla hiyo, Mbutuka iliwasilisha barua ya maombi ya hisa kwa Barrick na Rais wa Barrick Mark Bristow ametoa hati ya mwanahisa kwa Serikali na kumkabidhi Magufuli.

Kwa mujibu wa Waziri wa Mambo ya Nje, Profesa Palamagamba Kabudi amesema katika makubaliano hayo Serikali imepewa hisa asilimia 16 ambazo hazibadiliki hata kama Barrick itaongeza mtaji.

Rais  Magufuli akipeana mkono na Rais wa kampuni ya Barrick Dkt. Mark Bristow. 

Leave A Reply