The House of Favourite Newspapers

Tukutane kwa Mkapa

0

 

SIMBA imeamka! Wenyewe wanasema kwa mziki huu, tukutane kwa Mkapa Jumamosi ijayo tuoneshane makali jeuri ya Simba imekuja baada ya jana kuibuka na ushindi mnono wa mabao 5-0 dhidi ya Mwadui FC katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Uhuru, Dar.

 

Simba iliyotoka kupoteza mechi mbili mfululizo kwa kufungwa idadi sawa ya bao 1-0 dhidi ya Prisons na Ruvu Shooting, jana ilijipatia mabao yake kupitia kwa nahodha, John Bocco dakika ya 24 na 64 kwa pasi za Clatous Chama na Hassan Dilunga.

Mabao mengine ya Simba yalifungwa na Ibrahim Ajibu dakika ya 81 akimalizia pasi ya Dilunga, huku Dilunga naye akifunga bao la nne dakika ya 86 na Said Ndemla akahitimisha ushindi kwa bao la tano dakika ya tatu katika zile za nyongeza baada ya kutimia 90.

 

Ushindi huo wa jana kwa Simba ni kama salamu kwa Yanga ambapo watani hao wa jadi Jumamosi ijayo wanatarajiwa kupambana kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar ukiwa ni mwendelezo wa ligi hiyo mabingwa hao watetezi wamefi kisha pointi 16 na kupanda hadi nafasi ya tatu kutoka ya nne waliyokuwa awali wakifi kisha pointi 16 sawa na Biashara United.

 

Simba imecheza mechi nane, imeshinda tano, sare moja na kupoteza mbili.Katika mchezo wa jana ambao Simba ilionekana kuwa na hamu kubwa ya kuibuka na ushindi, kutokana na kosakosa nyingi walizozielekeza langoni mwa Mwadui, timu ambayo kwenye mechi mbili mfululizo imeruhusu mabao 11.

 

Ilifungwa 6-1 na JKT Tanzania, kabla ya jana kufungwa 5-0 na Simba.Chama ambaye hakuwepo kwenye mechi mbili zilizopita ambazo Simba ilipoteza, jana alionekana kuwa na makali akiwa na kiu kubwa ya kuisaidia timu yake na kurudisha furaha iliyopotea kwa siku kadhaa.

 

Kabla ya kuingia mabao hayo, dakika ya tisa tu ya mchezo, Luis Miquissone aliuweka mpira nyavuni, lakini halikuwa bao kwa kile kilichoelezwa alikuwa ameotea.Dakika 40, Luis alifanya hivyo tena na kukataliwa bao lake kutokana na kuotea kwa mara nyingine.

Mashabiki wa Simba walizomea ana kuona wanakataliwa mabao yao waliyodai yalikuwa halali Mwadui ilionekana kuzidiwa kwa kila kitu na kushindwa kupiga shuti lolote kwa muda wote wa dakika tisini za mchezo wa jana.

 

Miongoni mwa mashambulizi hatari ambayo Simba iliyafanya jana ni pamoja na Luis dakika ya 12 akiwa katika eneo la hatari, shuti lake lilipanguliwa na kipa wa Mwadui, Mussa Mbisa dakika ya 24, almanusura Bocco afunge bao, lakini mpira wa kichwa alioupiga akiunganisha krosi ya Mohammed.

 

Hussein, uligonga mlingoti wa goli na kurudi uwanjani, huku Said Ndemla shuti lake la dakika ya 33, lilidakwa kirahisi na kipa wa Mwadui kipa wa Simba, Beno Kakolanya, jana ilikuwa mechi yake ya pili ndani ya Ligi Kuu Bara msimu huu.

Ya Kwanza aliruhusu bao moja na jana hakuruhusu, hivyo ana clean sheet moja katika mchezo wa jana, Simba iliwatumia manahodha watatu, alianza Bocco, alipotoka akawa Chama ambaye naye alipotoka akamuachia mikoba Shomary Kapombe.

Leave A Reply