The House of Favourite Newspapers

Mbowe, Wenzake Mbaroni Tuhuma Kupanga Maandamano

0

KAMANDA wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, ACP Lazaro Mambosasa amesema wanawashikilia watu kadhaa wakiwemo viongozi wanne wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa tuhuma za kupanga maandamano.

 

Viongozi wa Chadema wanaowashikilia ni pamoja na mwenyekiti wa chama hicho taifa, Freeman Mbowe, Godbless Lema, Isaya Mwita (aliyekuwa Meya wa Jiji la Dar es Salaam) na Boniface Jacob aliyekuwa Meya wa Ubungo na mgombea ubunge wa Jimbo la Ubungo.

 

Amesema wanawashikilia viongozi hao kwa kuwa wanahatarisha usalama wa raia na mali zao kwa kuwa
wamepanga kuanza maandamano kitaifa yasiyokuwa na kikomo kuanzia Novemba 2, mwaka huu kwa kuwatumia vijana kuchoma moto miundominu na vituo vya mafuta.

 

“Mbowe na wenzake watashitakiwa kwa makosa ya ugaidi kwa sababu kuna mtu mtu ametupa ushahidi kuwa walipanga kulipua vituo vya mafuta jijini Dar na kuleta maafa makubwa.
“Uharamu wa maandamano haya hawakutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi, wanahamasishana chini kwa chini, kufunga barabara ili wananchi washindwe kufanya shughuli zao, hakuna atakayeruhusiwa kufanya mikusanyiko isiyo halali,” amesema Mambosasa.

Aidha, jeshi hilo linaendelea kuwasaka watu wanaowashawishi vijana kushiriki maandamano ambayo polisi wamesema ni ya vurugu kwa kuwa wanaoshawishiwa ni vijana wavuta bangi. Wengine wanaosakwa ni viongozi wa chama cha ACT Wazalendo.

 

Leave A Reply