The House of Favourite Newspapers

Jafo: Vibali Biashara Vyuma Chakavu Vitolewe kwa Miaka Mitatu

0

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Suleiman Jafo ametoa agizo kuwa vibali vyote vya ukusanyaji, usafirishaji na uhifadhi wa vyuma chakavu vitolewe kwa muda wa miaka mitatu na sio kwa mwaka mmoja kama ilivyokua awali ili kuepusha usumbufu kwa wawekezaji.

 

 

Ametoa agizo hilo alipokuwa katika ukaguzi kwenye kiwanda cha Metro Steel Ltd kinachozalisha nondo kilichopo Kiwalani jijini Dar es Salaam.

 

Akiwa katika kiwanda hicho, Jafo ametoa onyo kwa wenye viwanda kwa kutofuata sheria, taratibu na kanuni za mazingira. Pia ametoa rai kwa wenye viwanda kwa kulinda miundombinu ya Nchi na kutokufanya uharibifu katika kupata vyuma chakavu.

 

 

Amesema kiwanda hicho kinalalamikiwa na wananchi kuwa muda wa usiku kinatoa moshi na kusababisha kero kwa wakazi walio karibu na kiwanda hicho.

 

 

“Natoa onyo kali kwa kiwanda hiki leo sijaja kupiga faini ningeweza kumwambia Mkurugenzi Mkuu wa NEMC awapige faini ila ninawapa onyo mjirekebishe katika hili”. amesema Jafo.

 

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa NEMC Dk. Samuel Gwamaka, amesema kiwanda cha Metro Steel kina kibali cha usafirishaji lakini kibali hakina tarehe wala kiasi cha chuma chakavu kilichosafirishwa na kushushwa kiwandani.

 

 

“Utaratibu uliopo lazima kibali kiandikwe tarehe na kiasi cha chuma chakavu kinachosafirishwa na vinginevyo kutoandikwa tarehe kibali kimoja kinaweza kutumika bila kikomo hivyo kuwa na kibali kisichoandikwa tarehe ni makosa”. amesema Dk. Gwamaka.

Leave A Reply