The House of Favourite Newspapers

Gazeti la Championi Latoa Tiketi Kwa Mashabiki wa Simba/Yanga

0
Mkuu wa Idara ya Usambazaji wa Global Publishers (kushoto) akipozi na msomaji wa gazeti la Championi ambaye ni shabiki wa timu ya Simba.
Shabiki wa timu ya Simba akionesha Gazeti la Championi pamoja na tiketi aliyokabidhiwa kutoka kwa maofisa masoko wa Global Publishers.
Mkuu wa Idara ya Usambazaji wa Global Publishers (kulia) akimkabidhi shabiki wa Timu ya Simba tiketi kwa ajili ya kuingia mechi ya Simba dhidi ya Yanga.
Ofisa Masoko wa Kampuni ya Global Publishers, Songolo Bilaly (kushoto) akimkabidhi tiketi.
Ofisa Masoko wa Kampuni ya Global Publishers, Songolo Bilaly (kushoto) akimkabidhi tiketi shabiki wa timu ya Yanga.
Mkuu wa Idara ya Usambazaji wa Global Publishers (kulia) akimkabidhi tiketi msomaji wa gazeti la Championi kwa ajili ya kuingia mechi ya Simba dhidi ya Yanga.

KAMPUNI ya Global Group kupitia gazeti namba moja la michezo Tanzania, Championi limetoa zawadi za tiketi kwa wateja wake ili waweze kushuhudia mtanange wa leo kati ya Simba na Yanga.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa leo saa 1:00 usiku Uwanja wa Mkapa unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na utani wa jadi wa timu hizi mbili.

 

Ni mashabiki wa Simba na Yanga ambao walikutwa na timu ya usambazaji wakisoma gazeti la Championi Jumamosi waliweza kupewa zawadi ya tiketi ya mchezo huo.

Anthon Adam, Mkuu wa Kitengo cha Usambazaji kutoka Global Group amesema kuwa ni kawaida ya kampuni hiyo kurudisha fadhila kwa wasomaji wake kwa kuwapa tiketi hizo ikiwa ni pamoja na zawadi mbalimbali ambazo kampuni hiyo imekuwa ikizitoa.

 

“Hii imekuwa desturi yetu kurudisha fadhila kwa wasomaji wetu kwani wamekuwa wakituunga mkono, hivyo ni jambo jema kuwarudishia kile tunachokipata kutoka kwao, kwa kuwa sote ni familia ya Championi.

 

“Wasomaji wetu tuliowakuta wakiwa na nakala ya gazeti la Championi Jumamosi tumewapa tiketi ya kwenye mechi ya Simba dhidi Yanga, hii imekuwa ni kawaida yetu kuwapa tiketi wasomaji wetu wanaokutwa wakiwa na nakala ya gazeti,” amesema.

Leave A Reply