The House of Favourite Newspapers

Yanga Yakubali Muziki wa Simba

0

KAIMU Mtendaji Mkuu wa Yanga, Senzo Mbatha Mazingisa, amefunguka kuwa anaipongeza Simba kupitia kwa Mtendaji Mkuu Barbara Gonzalez kwa kufanikiwa kupata wadhamini wengi kwa wakati mmoja.

 

Senzo amesema wanachofanya Simba ndicho kinapaswa kufanywa na klabu zote Tanzania na mpira wa Tanzania unatakiwa kwenda huko kwa hiyo Simba na viongozi wake wanapaswa kupongezwa kwa hatua hiyo waliyofikia.

 

Akizungumza na Championi Jumatatu, Senzo alisema haoni kosa kuwasifu Simba kwa hatua nzuri waliyofikia kwa sababu ndiyo maendeleo ya soka la kisasa kwa sababu timu ikiwa na vyanzo vingi vya mapato inaimarika zaidi.

 

“Nawapongeza Simba na mtendaji wake Barbara kwa kufanikiwa kupata wadhamini wengi kwa muda mfupi. Mara nyingi nimekuwa nikizungumza juu ya maendeleo ya soka hapa nchini na Afrika timu zetu lazima zifike huko kwa kuwa maendeleo ya soka la kisasa ndiyo yanataka hivyo,” alisema Senzo.

 

Senzo alipoulizwa kuhusu Yanga lini watafanya kama Simba alijibu kuwa siyo lazima Yanga waige kila kitu ambacho Simba wanafanya.

 

“Hiyo ndiyo shida ya soka la Tanzania, Simba na Yanga hawatakiwi kufanya kila kitu kiwe sawa, haiwezekani Simba kapata wadhamini wa mabasi na sisi tutafute haohao, haiwezi kuwa sawa.

 

“Yanga tuna mipango yetu na njia zetu za kupata wadhamini au kufikia malengo yetu, utani wa jadi na Simba hauwezi kuwa sababu ya Yanga tuanze kufanya kama wao,” alisema Senzo.

ISSA LIPONDA, Dar es Salaam

Leave A Reply