The House of Favourite Newspapers

Uzinduzi wa Awali wa Rifaly Badala ya M-Paper

0
Wadau wakiwa katika mjadala juu ya ujio mpya wa huduma za Rifaly na faida zake.

Dar es Salaam, Tanzania 18 Januari 2023: Kampuni ya Smart foundry imezindua bidhaa yake mpya iitwayo ‘Rifaly’ ambayo ni jina jipya la bidhaa yao ya ‘M-Paper’.

Rifaly ni App ya kuuza maudhui ya Kiafrika kuanzia magazeti, majarida, vitabu, makala na hadithi za sauti. Hii inakuja kama toleo jipya la M-Paper ambayo hapo awali ilitoa magazeti na majarida tu kwa wateja wake.

Wadau wakisikiliza kiumakini.

Programu ya Rifaly ni program inayowapatia watu maudhui ya Kiafrika kuanzia magazeti, majarida, vitabu, nakala, na hadithi za sauti.

Hii inakuja kama ongezeko la program ya awali iliyojulikana kama M-Paper ambayo iliwapatia wateja wake magazeti na majarida kidijitali.

Tunafurahi kuwaalika waandaaji wa maudhui maarufu kama “content creators” kujiandikisha na kushiriki katika kuwafikishia wateja wetu maudhui yaliyo katika mfumo wa kidijitali, na kuwafikia watu wengi zaidi.

“Alisema Edwin Bruno CVO wa Smart Africa Group wakati wa majadiliano ya jopo.

Mkuu wa Smart Foundry Bwana Johannes Lutainulwa, aliweza kutoa mwanga zaidi juu ya utumiaji na huduma za programu, alielezea kuwa aplikesheni ya RIFALY, itawawezesha vijana wa Kitanzania ambao ni waandaaji wa maudhui kuwapatia jukwaa lililotengenezwa hapahapa nyumbani ambapo wanaweza kupata thamani kubwa kwa kazi yao ya kidijitali, iwe ni simulizi za sauti, vitabu, magazeti, au majarida”.

Katika awamu ya kwanza, Aplikesheni hii ya Rifaly kwasasa inatoa hadithi za sauti kama huduma mpya na kuendelea na magazeti na majarida.

Vitabu na nakala zinatarajiwa kuongezwa kwenye program ifikapo katikati ya mwezi wa Februari mwaka huu. Alimaliza kusema Mkuu wa Smart Foundry Bwana Johannes.

Leave A Reply