The House of Favourite Newspapers

DCI Ramadhani Kingai Atembelea Ocean Road,”Polisi nao Ni Wanajamii”

0

Askari Polisi alijiunga na Jeshi la Polisi na kuhudhuria mafunzo ya awali mwaka 2000/2001 leo wametembelea Taasisi ya Saratani Ocean road na kutoa misaada kama sadaka kwa wagonjwa wanaougua maradhi ya saratani ikiwa ni namna ya kumshukuru Mungu kwa afya na uzima katika kipindi chote cha kazi tangu walipojiunga na Jeshi la Polisi.

Akiongea na waandishi wa habari kwa niaba ya maofisa, wakaguzi na askari Polisi walipotembelea
hospitalini hapo Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya jinai (DCI), Kamishna wa Polisi, Ramadhani
Kingai amesema kwamba misaada hiyo imetokana na michango ya askari hao ambao walichanga na
kununua zawadi kwa watu wenye uhitaji kama wagonjwa.


Aidha, Kamishna Kingai amesema sadaka ni jambo ambalo linatimiza maelezekezo ya Mungu kutoka katika vitabu vitakatifu kwa kuwahurumia watu wenye uhitaji hivyo wanachi watambue kwamba Askari Polisi ni miongoni mwa wanajamii ambao wanajali an kuwathamini. hivyo wanawaombea wapone ili waweze kuendelea na shughuli zao za kimaendeleo.

Akiongea kwa niaba Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi Saratani Ocean Road, Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Taasisi ya Saratani Ocean Road Dkt. Mark Athumani Mseti ameshukuru kwa misaada iliyotolewa na kwa uamuzi mzuri wa Askari hao kutembelea hospitalini hapo na kwamba hilo limeonesha kwamba Jeshi la Polisi halipo kwaajili ya kulinda raia na mali zao tuu bali hata kujali afya za raia wa Tanzania, na kuwaomba wananchi wanapotakiwa kutoa taarifa za wahalifu watoe taarifa ili Jeshi la Polisi lizidi
kufanya kazi kwa ufansi zaidi.


Misaada hiyo imehusisha baadhi ya vifaa tiba, sabuni za kufulia na kuogea, nguo, vitenge, vyandarua, miswaki, dawa za meno, kandambili, Pampas, mafuta ya kupaka na maji ya kunywa.

 

Leave A Reply