The House of Favourite Newspapers

Usipige Bwana…Tuma Meseji!-2

0

Ilipoishia Wiki Iliyopita:

Asubuhi, Bony ndiye alitangulia kuamka, akakaa sebuleni akiangalia habari za ulimwengu kwenye runinga kupitia BBC. Mkewe alipotoka chumbani, akamuuliza kama Aisha alishaaamka…

“Sijamwona, labda kama kaamka halafu amerudi kulala ndani,” alisema Bony huku macho yakikaza kwenye runinga.

Neema alirudi chumbani kwake, akaoga, akajiandaa kwenda kazini.

JIACHIE MWENYEWE…

 

Baby, sitaki kumsumbua mke mwenzangu, akitoka mwambie aingie jikoni kila kitu kipo kwa ajili ya asubuhi hii na mchana pia kama nitachelewa kurudi,” alisema Neema akiwa na mkoba wake kwenye kwapa, mkononi ameshika funguo za gari…

“Sawa,” alikubali Bony…

“Oke darling, basi baadaye mwambie Aisha nimemwachia nyumba na mume pia.”

“Kazi njema mke wangu,” alisema Bony huku akicheka kwani siku zote katika familia hizo, utani wao mkubwa ni huo. Bony akienda nyumbani kwa Mudy, humtania Aisha ni mke wake huku Mudy mwenyewe akiwepo.

Mudy naye akienda nyumbani kwa Bony humtania Neema kwamba ni mke wake, Bony mwenyewe akiwepo. Na wanawake nao, kila mmoja mume wa mwenzake anamwita mume wake yeye.

***

Aisha aliamka akiwa amechoka sana kwani usingizi wenyewe ulimpata saa tisa alfajiri. Alikuwa macho kutokana na kubadili ghafla mazingira. Kutoka kulala na mumewe, Mudy mpaka mwenyewe tena nyumbani kwa mtu…

“Ha! Shem za asubuhi?” alisalimia Bony akiwa ameachana na tivii sasa akawa anamwangalia Aisha…

“Salama shemeji, umeamkaje?”

“Aaa! Mimi nimeamka salama sana, pole na uchovu, pole na mazingira mageni.”

“Ni kweli shemeji, mazingira ni mageni. Usingizi umenijia saa tisa kama sikosei. Halafu si unajua mazoea? Unalala ukiweka mkono nyuma unamgusa mwenzako, sasa leo nimelala nikiweka mkono hivi nakutana na mto tu,” alifunguka Aisha huku akikaa kwenye kochi kubwa.

“The! The! The! Pole sana shemeji. Lakini ndani ya kipindi kifupi sana utazoea na utakuwa kama kawaida,” Bony alimpa moyo shemeji yake…

“Namwomba Mungu iwe hivyo shemeji…vipi Neema?”

“Neema ameshakwenda kazini. alisema anahisi umechoka asikusumbue. Lakini kasema ukiingia jikoni kila kitu kipo.”

“Aha! Jamani! Angeniamsha tu. Kukikucha kumekucha tu, hata iweje…oke, ngoja basi nikaoge. Lakini wewe si huendagi kazini siku ya leo?” Aisha alisema na kutembea kuelekea bafuni…

“Mimi nipo leo shem…kama wewe tu.”

Aisha asubuhi hiyo alikuwa amejifunga kanga moja tu kwa kuizungushia kwenye nido zake na juu yake akapitisha taulo kwa kulizungushia kiunoni.

“Kwa kweli kitendo cha mume wangu Mudy kuondoka ni bonge la pengo, kwanza usiku wa leo nilikuwa mpweke mno na muda huu tungekuwa tunaoga wote na kucheza huku bafuni,” Aisha aliwaza

Baada ya kutoka kuoga, Aisha aliingia chumbani kwake, akabadili nguo. Akavaa suruali ya skin’taiti nyeusi na kitop cheupe. Umbo lake lilikuwa sawia. Kila eneo lilijidhihirisha lenyewe. Bastola, kifua, miguu, kiuno, nido na sehemu nyingine zote.

Alikwenda jikoni, akaandaa chai na kuitenga kwenye meza ya kulia chakula. Ilikuwa chai yenye mikate na mayai maarufu kwa jina la jicho la ng’ombe huku pembeni kukiwa na sahani yenye vipande vya nyama ya kukaanga.

“Shem karibu chai,” Aisha alimkaribisha Bony kwa heshima zote…

“Du! Afadhali shem, maana tumbo lilishaanza kunguruma likidai chochote,” Bony alitania kidogo, Aisha akacheka huku akitangulia kwenye meza.

Aisha alimmiminia chai Bony, akamuwekea sukari huku akimwambia…

”Najua wewe ni vijiko viwili tu tosha…uongo?”

“Haswa! Nikizidisha hapo nakosa hamu kabisaaa.”

Aisha alicheka, Bony naye akacheka…

“Mbona unacheka shem?” aliuliza Bony licha ya kwamba na yeye alicheka…

“Nimecheka shem wangu kwa sababu umenijulia kuhusu sukari.”

“Jamani! Kila mke anamjua mume wake na mume naye anamjua mke wake. Sasa nitashindwa kukujulia mume wangu?”

“Kweli kabisa mke wangu…wewe ni mke mwema.”

Walikuwa wakinywa chai huku sasa wakiwa siriasi na mazungumzo mengine …

“Hivi shem, wale wanaotengana na wake zao kwa miaka mitatu kwa sababu wamekwenda kusoma huwa wanawezaje? Maana mimi kusema kweli mwaka mmoja halafu leo ndiyo siku ya kwanza, kwangu naona kama Mudy amefariki dunia tu,” alisema Aisha…

“Kwa hiyo kama unaona Mudy amefariki dunia unataka kuolewa tena?” Bony aliuliza kwa utani, Aisha akacheka…

“Siyo hivyo shem. Sasa mwaka mmoja jamani! Mimi nitaishije huku?”

“Utaishi tu. Si ndiyo maana amekuacha kwangu shem, alijua unaweza kukosa hata pesa ya kula, mimi nipo, utakula. Unaweza kukosa pesa ya kuweka mafuta kwenye gari, mimi nipo…”

“Shemeji ninachosemea mimi nitaishije ni tofauti na vyote hivyo ulivyovisema wewe,” alifunguka Aisha…

 

Je, nini kiliendelea hapo? Usikose kusoma chombezo hili jipya kwenye Gazeti la Ijumaa Wikienda, Jumatatu ijayo.

Leave A Reply