The House of Favourite Newspapers

Real Madrid Walivyotwaa Kombe la UEFA (Video+Picha)

0

uefa finale (15) uefa finale (16) uefa finale (17) uefa finale (18) uefa finale (19) uefa finale (20) uefa finale (21)
uefa finale (1) uefa finale (2) uefa finale (3) uefa finale (4) uefa finale (5) uefa finale (6) uefa finale (7) uefa finale (8) uefa finale (9) uefa finale (10) uefa finale (11) uefa finale (12) uefa finale (13) uefa finale (14)
Kikosi cha Real Madrid kimefanikiwa kutwaa Kombe la Ligi ya Mabingwa barani Ulaya kwa kuwachapa mahasimu wao Atletico Madrid kwa penalti 5-3 baada ya dakika 120 kukamilika kwa sare ya 1-1 kwenye mechi hiyo ya fainali iliyopigwa Uwanja wa San Siro jijini Milan nchini Italia.

Bao la Real Madrid katika muda wa kawaida lilifungwa na Sergio Ramos dakika ya 15 huku Atletico Madrid wakisawazisha dakika ya 79 kupitia kwa Yannick Carrasco na kufanya matokeo kuwa 1-1.

Dakika 90 zilimalizika kwa sare ya 1-1 na kuongezwa dakika 30 ambazo nazo zilimalizika bila timu hizo kuongeza mabao na kuamriwa ipigwa mikwaju ya penalti ambapo Real waliibuka kidedea kwa penalti 5 huku Atletico wakifunga 3.

Real Madrid waliofunga penalti ni;

1.Vazquez
2.Marcelo
3.Bale
4.Ramos
5.Ronaldo

Atletico Madrid;

1. Griezman
2. Gabi
3. Saul
4. Juanfran (alikosa)
5.

Kwa matokeo hayo, Real Madrid wanaendelea kuongoza wakiwa wamelichukua kombe hilo mara 11
mwaka 1956, 1957, 1958, 1959, 1960, 1966, 1998, 2000, 2002, 2014, 2016 huku wakifuatiwa na AC Milan waliolitwaa mara 7 kombe hilo mwaka 1963, 1969, 1989, 1990, 1994, 2003, 2007 na Bayern Munich wapo nafasi ya tatu wakiwa wamelitwaa mara 5 mwaka 1974, 1975, 1976, 2001, 2013.

Vikosi katika fainali hiyo vilikuwa;
Real Madrid (4-3-3): Navas; Carvajal (Danilo 51), Ramos, Pepe, Marcelo; Casemiro, Kroos (Isco 72), Modric; Bale, Ronaldo, Benzema (Lucas 76).

Benchi: Nacho, Rodriguez, Casilla, Jese

Kadi za njano: Carvajal, Navas, Casemiro, Ramos, Danilo, Pepe

Kocha: Zinedine Zidane

Atletico Madrid (4-4-2): Oblak; Juanfran, Savic, Godin, Filipe Luis (Gomez 109); Saul, Gabi, Augusto (Carrasco 46), Koke (Thomas 116); Griezmann, Torres.

Benchi: Moya, Mendes, Correa, Gimenez

Kadi za njano: Torres, Gabi

Kocha: Diego Simeone

Leave A Reply