Rasmi Kwasi Arithi Mikoba ya Banda Sauzi

HATIMAYE aliyekuwa beki wa Simba, Mghana Asante Kwasi amejiunga na Baroka FC inayoshiriki Ligi Kuu ya Afrika Kusini timu aliyokuwa akiitumikia Mtanzania, Abdi Banda kabla ya hivi karibuni kutua Highland Parks ya nchini humo.

 

Kwasi ni mmoja wa wachezaji wa Simba ambao wameachwa katika dirisha la usajili baada ya kumaliza mkataba. Simba ilimsajili Mghana huyo akitokea kwenye Klabu ya Lipuli, ambapo hapo awali aliwahi kuzitumikia Mbao FC na Mbabane Swallows ya Eswatin.

 

Mtandao mmoja kutoka nchini Afrika Kusini, umeripoti kuwa: “Hatimaye Klabu ya Baroka imefikia muafaka na kumsajili aliyewahi kuwa beki wa Simba, Asante Kwasi raia wa Ghana ambaye ametua kama mchezaji huru.”

 

Kwasi atakuwa ni mchezaji wa pili wa Simba kutua katika Ligi Kuu ya Afrika Kusini baada ya hivi karibuni kiungo, James Kotei kujiunga na Kaizer Chiefs.


Loading...

Toa comment